Mtakatifu Marko
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Marko)
Mtakatifu Marko (kwa Kilatini Mārcus; kwa Kigiriki Μᾶρκος) aliishi katika karne ya 1 BK. Alikuwa Myahudi wa Yerusalemu aliyeongokea mapema Ukristo pamoja na Maria mama yake. Kanisa la kwanza lilikuwa linakusanyika nyumbani mwao.
Alifanya kazi na mitume Paulo na Barnaba katika kuhubiri Injili huko Kupro na Uturuki.
Baadaye alikuwa na Mtume Petro na Paulo katika mji wa Roma hadi walipouawa na serikali ya Kaisari Nero (64-67).
Ndipo alipoandika Injili ya kwanza, iliyofuatwa na Mtume Mathayo na Mwinjili Luka, ingawa katika orodha za Biblia inashika nafasi ya pili.
Kadiri ya mapokeo alifariki wakati akifanya kazi hiyo huko Alexandria nchini Misri.
Marejeo [hariri]
- The Apostle and Evangelist Mark (40–62). Official web site of the Greek Orthodox Patriarchate of Alexandria and All Africa. Rudishwa juu ya 2011-02-07.
Viungo vya nje [hariri]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
- The Life, Miracles and Martyrdom of St. Mark the Evangelist of Jesus Christ
- H.B. Swete, 'St. Mark in the New Testament'
- H.B. Swete, 'St. Mark in Early Tradition'
- St. Mark the Apostle, Evangelist, and Preacher of the Christian Faith in Africa
Joseph MacRory (1913). "St. Mark". Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company.- Apostle Mark the Evangelist of the Seventy Orthodox icon and synaxarion
| Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mtakatifu Marko kama historia yake au athari wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
