Maria Ana wa Yesu
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mchoro wa Francisco Sylverio de Sotomayor (karne ya 18) kuhusu Mariana de Jesús, Azucena de Quito, Heroina Nacional y Virgen Penitente.
Maria Ana wa Yesu (jina kamili la Kihispania ni Mariana de Jesús Paredes y Flores) alizaliwa Quito (Ekwador) tarehe 31 Oktoba 1618 akafariki huko tarehe 26 Mei 1645.
Bikira huyo wa Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu tangu tarehe 4 Juni 1950, alipotangazwa na Papa Pius XII. Kabla yake, Papa Pius IX alikuwa amemtangaza mwenye heri tarehe 20 Novemba 1853.
Ni mtu wa kwanza kutoka Ekwador, na Mfransisko wa kwanza kutoka Amerika Kusini kutangazwa mtakatifu.
Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe 26 Mei.
Viungo vya nje[hariri]
- Mary Anne de Paredes|work=Catholic Encyclopedia
- Mary Ann of Jesus of Paredes |work=American Catholic
- ANN de Paredes|work=Catholic Forum
- GENEALOGÍA. Orígenes familiares de Santa Mariana de Jesús y descendencia de sus hermanos en la base de datos para Ecuador de Mauricio Alvarado-Dávila.
- Nota biográfica por Gustavo Amigó Jansen
- Poema que le dedicó Hernando de la Cruz
| Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Maria Ana wa Yesu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |