Margaret Okayo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Margaret Okayo

Margaret Okayo (alizaliwa Masaba (Migori), 30 Mei 1976) ni mwanariadha wa mbio za marathon aliye na ufanisi mkuu nchini Kenya. Ameshinda mataji mengi katika mbio hizo.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Aligundua talanta yake ya riadha akiwa katika shule ya msingi. Alisoma katika Shule ya Sekondari ya Itierio, iliyomo mjini Kisii mnamo 1993. Alijiunga na kitengo cha askari wa magereza cha Kenya mnamo 1995, ambapo aliendelea kuitunza talanta yake.

Mashindano[hariri | hariri chanzo]

Mnamo 1998 wakati wa Mashindano ya Olimpiki Okayo alimaliza wa tano katika shindano la mita 10000. Alimaliza wa 13 katika mashindano ya IAAF Half Marathon ya 1999. Miongoni mwa mashindano yake ya ufanisi zaidi ni Mashindano ya en:New York Marathon ya 2003 na Boston Marathon ya 2002. Katika mashindano yote anashikilia rekodi. Aliweka Rekodi mpya katika katika masafa ya Marathon mnamo 4 Novemba 2001 katika mji wa New York, lakini haishikilii sasa hivi. Mashindano mengine ya Marathon aliyoyashinda ni London Marathon ya 2004, Milan Marathon ya 2003, San Diego mnamo 2000 na 2001. Aliiwakilisha nchi yake ya Kenya katika mashindano ya Olimpiki ya 2004- Shindano la wanawake la Marathon. Yeye hutumia miezi mitatu kila mwaka kujifunza kule Italia. Alishinda katika mashindano ya Udine Half Marathon ya mwaka wa 2003[1] na kumaliza wa tatu katika mashindano ya Rome-Ostia Half Marathon ya 2008[2].

Mengine kumhusu[hariri | hariri chanzo]

Okayo anatoka katika jamii ya Kisii. Meneja wake ni Federico Rosa na Kocha wake ni Gabriele Rosa. Ana urefu wa mita 1.52 na uzani wa kilo 43.

Rekodi za Marathon[hariri | hariri chanzo]

Tazama Pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]