Maretadu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Kata ya Maretadu
Nchi Tanzania
Mkoa Manyara
Wilaya Mbulu
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 21,158

Maretadu ni kata ya Wilaya ya Mbulu Vijijini katika Mkoa wa Manyara, Tanzania.

Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 14,343 waishio humo.[1]

Kata ya Maretadu hata hivyo ina vijiji kama Endamasak, Maretadu Juu, Maheri, Qamtananat, Maretadu Chini na Garkawe.

Wakazi wa Kata ya Maretadu hasa ni wa makabila ya Wairaqw na Watatoga.

Shughuli kubwa ya kiuchumi ya wakazi wa hapo ni kilimo na ufugaji. Kilimo kinachoendeshwa sana ni cha mahindi, maharage, ngano, dengu, alizeti, mtama, n.k. Ufugaji ni wa ngombe, mbuzi, kondoo, punda na kuku.

Hali ya hewa huko ni nzuri yenye misimu ya mvua na ya kiangazi kwa muda unaoeleweka. Masika huanza mwezi Novemba - Mei. Baada ya hapo ni kiangazi na vuli za kawaida.

Kata ya Maretadu ina shule kadhaa za msingi kama Maretadu juu, Maretadu Chini, Hayedarer, Simha, Qamtananat. Shule ya Msingi Maretadu Juu ni ya miaka mingi na imeanza mwaka 1953. Tokea hapo imeendelea kutoa wasomi wengi na inafanya vizuri hadi sasa.

Pia kuna Shule za Sekondari kama Shule ya Sekondari Maretadu, shule ya Sekondari Maretadu Juu, na Shule ya Sekondari Jakaya Kiwete. Wasomi kadhaa wametoka katika kata hiyo. Baadhi ni Prof. Joshua Doriye aliyepata kushika nyadifa mbalimbali Serikali hadi ngazi ya Katibu Mkuu wa Wizara, Tume ya Mipango na Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Dar es Salaam. Pia yuko Dr. Bertha Maegga, wa Taasisi ya Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu (NIMRI).

Maretadu hata hivyo inahitaji maendeleo katika nyanja mbalimbali ili ipate kusonga mbele kutoka hapo ilipofikia.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Kata za Wilaya ya Mbulu Vijijini - Mkoa wa Manyara - Tanzania

Bashay | Dinamu | Dongobesh | Endamilay | Eshkesh | Geterer | Gidhim | Haydarer | Haydom | Labay | Maghang | Maretadu | Masieda | Masqaroda | Tumati | Yaeda Ampa | Yaeda Chini


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Manyara bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Maretadu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.