Marcia Cross

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Marcia Cross

Marcia Anne Cross (alizaliwa 25 Machi 1962) ni mwigizaji wa Marekani. Anajulikana katika uigizaji kama mhusika wa Bree Van de Kamp kwenye kipindi cha Desperate Housewives.

Masomo na Uigizaji[hariri | hariri chanzo]

Marcia Cross alisoma shule ya msingi na ya upili katika shule ya Juilliard mjini New York, na kisha akafuzu kwa shahada ya pili ya saikolojia kutoka kwa chuo kikuu cha Antioch mjini Los Angeles. Alianza kuigiza mnamo 1984 kwenye kipindi cha The Edge of Night. Baadaye, aligura kutoka mji wa New York hadi Los Angeles na kisha akaigiza kwenye filamu ya The Last Days of Frank and Jessie James. Kuanzia 1986 hadi 1987, aliigiza kama Kate Sanders kwenye kipindi cha One Life to Live.

Mnamo 1992, Cross aliigiza kama Dkt. Kimberley Shaw kwenye kipindi cha Melrose Place. Hapo awali, alikuwa amepewa mkataba wa kuigiza kwenye kipindi hiki kwa muda wa msimu mmoja, lakini aliwafurahisha watayarishaji wakuu hadi wakakubali kumweka mpaka msimu wa nne.

Baada ya kuwacha Melrose Place, Cross alijiunga na kipindi cha Seinfield ambapo aliigiza kama Dkt. Sitarides. Pia, ameigiza kwenye vipindi kama CSI: Crime Scene Investigation, Profiler, Everwood na Touched by an Angel.

Mnamo 2004, Cross alifaulu kujiunga na kipindi cha Desperate Housewives.

Maisha ya kibinafsi[hariri | hariri chanzo]

Cross alizaliwa mjini Marlborough, Massachusetts. Yeye alikuwa rafiki wa dhati wa Richard Jordan. Jordan alikuwa mkubwa wa Cross kwa miaka ishirini na tano. Yeye alikufa kutokamana na uvimbe wa bongo mnamo 1993.[1]

Cross aliolewa na Tom Mahoney mnamo 24 Juni 2006.[2] Mnamo 6 Septemba 2006, alitangaza kuwa yeye ni mjamzito. Mnamo 20 Februari 2007 Cross alijifungua pacha: Eden na Savannah katika hospitali mjini Los Angeles.[3]

Filamu[hariri | hariri chanzo]

  • The Edge of Night (1984), Liz Correll
  • Brass (1985), Victoria Willis
  • One Life to Live (1985-86), Kate Sanders
  • Tales From The Darkside (1986), Strange Love
  • The Last Days of Frank and Jesse James (1986), Sarah Hite
  • Almost Grown (1988-1989), Lesley Foley
  • Cheers (1989), Susan Howe
  • Bad Influence (1990), Ruth Fielding
  • Storm and Sorrow (1990), Marty Hoy
  • Knots Landing (1991-1992), Victoria Broyelard
  • Murder, She Wrote (1992), Marci Bowman
  • Ripple (1995), Ali
  • Melrose Place (1992-1997), Dkt. Kimberly Shaw Mancini
  • Always Say Goodbye (1996), Anne Kidwell
  • Female Perversions (1996), Beth Stephens
  • All She Ever Wanted (1996), Rachel Stockman
  • Seinfeld (1997), Dkt. Sara Sitarides
  • Target Earth (1998), Karen Mackaphe
  • Boy Meets World (1999) , Rhiannon Lawrence, Topanga's mother (4 episodes)
  • Dancing in Septemba (2000), Lydia Gleason
  • Profiler (2000)
  • Living in Fear (2001), Rebecca Hausman
  • CSI: Crime Scene Investigation (2001), Julia Fairmont
  • Eastwick (2002), Jane Spofford
  • King of Queens (2002), Debi
  • Everwood (2003), Dkt. Linda Abbott
  • The Wind Effect (2003), Molly
  • Desperate Housewives (2004–hadi leo), Bree Hodge

Tuzo[hariri | hariri chanzo]

  • Mnamo 2006, alishinda tuzo la Screen Actors Guild Award (Outstanding Ensemble in a Comedy Series)
  • Mnamo 2005, alishinda tuzo la Screen Actors Guild Award (Outstanding Ensemble in a Comedy Series
  • Mnamo 2006, alishinda tuzo la Satellite Award (Best Actress in a Television Series - Musical or Comedy)

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Notice of death of Richard Jordan
  2. Wihlborg, Ulrica."Marcia Cross Gets Married." Archived 1 Aprili 2016 at the Wayback Machine. People. 24 Juni 2006.
  3. Gee, Alison. "Marcia Cross Welcomes Twin Girls" Archived 8 Machi 2013 at the Wayback Machine. People. 21 Februari 2007.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Marcia Cross kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.