Mapendo ya kiuchumba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Mapendo ya kiuchumba ni aina mojawapo ya mapendo kati ya binadamu. Katika maana halisi aina hiyo ni ya maandalizi kwa ajili ya ndoa.

Hapo zamani mara nyingine hapakuwepo na mapenzi ya kiuchumba kwani mvulana na msichana walifikia kuoana bila ya kuwepo kwanza uchumba.

Lakini kwa sasa, kutokana na maendeleo na akili kupanuka zaidi, kwa kawaida hakuna anayeoa au anayekubali kuolewa bila ya kumfahamu mchumba wake kwanza.

Ule muda wa kuzoeana, ndio wa mapendo ya kiuchumba, kwani haitoshi tu kumtamkia mpenzi wako kwamba ungependa awe mama watoto wako bila ya kuzijua silika, tabia, hisia zake na kadhalika.

Muda wa kuchumbiana ndio muda ambao wote wawili watakiwa kuwa makini sana kila mmoja kumsoma mwenzie na kujirekebisha ili kuwezesha ndoa kudumu hata itakapojaribiwa na maisha.