Makeni
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Makeni ni mji nchini Sierra Leone na makao makuu ya Mkoa wa Kaskazini pia penye utawala wa wilaya ya Bombali.
Idadi ya wakazi ni takriban watu 94,000 (kadirio 2007). Mji ulijulikana nchini kwa sababu ya soko lake na msikiti mkubwa. Katika vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Sierra Leone uliathiriwa vibaya na kuona uharibifu wa nyumba nyingi. Wanamigambo wa upinzani walikuwa na makao makuu yao mjini hapo.
Makeni iko takriban 120 km kaskazini ya mji mkuu Freetown. Rais Ernest Bai Koroma alizaliwa mjini.