Majadiliano:Uzinifu

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

kuna faida za kutoingia katika zinaa na mke/mume mtarajiwa kwangu?[hariri chanzo]

Kwanza kabisa ni vema kujua ya kwamba Mungu wetu mwenyezi,yeye mwenye uwezo wote ana uwezo na alikuwa nao wakutuumba bila matamanio ya kimaumbile kati ya mwanamume/mvulana na mwanamke/msichana,bali kwa makusudi kabisa hakutaka binadamu awe mpweke na alipenda liwepo tendo la ndoa ilimradi katika maisha wawili yaani mke na mume waweze kushirikiana na kuheshimiana kwakuwa umuhimu wa kila mmoja unadhihirika kwa kila mmoja kuumbwa tofauti na mwenzake hasa katika nyanja ya maungo ya kiume au yakike,hivyo mwanamume atamwitaji mwanamke na atakuwa mkamilifu vivyo hivyo na mwanamke kwa maana iliandikwa mwanamume atawaacha wazazi wake,naye ataambatana na mkewe nao watakuwa mwili mmoja kuwa mwili mmoja inamaana mwanamume hawezi kujitosheleza na mwanamke hawezi kujitosheleza mahitaji ya hisia za mwili wake kwa namna impendezayo Mungu bila mwenza wa ndoa. Kwa dhumuni hilo la Mungu,ni zawadi kwa mwanadamu katika maisha ya ambayo Mungu amemuumbia.Kama tu zawadi tunavyoipa heshima kuitunza kwa ajili ya mpewa wa hiyo zawadi,Mungu kwa kujua kabisa zawadi hiyo japo ni kwa ajili yetu ila anataka atupe katika muda ambao utakuwa ni mzuri na tumejiandaa kukabiliana na matokeo ya kupewa zawadi hiyo ambayo inaambatana na majukumu ya kulea watoto wanaotokana na kufurahia zawadi ya tendo la ndoa.Hivyo hakuna mtu atakayemchukiza Mungu kwa habari ya zinaa akiamua kufuata utaratibu mzuri uliowekwa kuipata hiyo zawadi. Hivyo kama wawili wamejiona wako tayari kupokea zawadi,hakuna haja ya kumwibia mwenye zawadi(Mungu)na kuamini atafurahishwa wakati hajaitoa kwao kwa kuamua bali kwa kunyang'anywa.Hasira ya kukuta mtu uliyetaka kumpa zawadi ameiba na kuitumia naamini kibinadamu tu ni kutokuwa na moyo wa kumwandalia mtu huyo zawadi kwa mara nyingine. Hivyo tukumbuke tunamchukiza Mungu kuanza tendo la ndoa kabla hivyo hata zawadi nyingine ambazo ni baraka katika maisha hayo ya ndoa tunakuwa tunazipoteza kwa kosa dogo la kupora kinachokustahili badala ya kujiweka tayari na kuiomba maana hakuna imani yoyote au kanisa lolote litakalokataa kuwaunganisha wawili waliokwenda kupata muunganiko unaotambulika na Mungu ili waweze kupokea hiyo zawadi. Shetani akiwa ni adui kwetu tangu atimuliwe mbinguni,amekuwa na kisasi na Mungu na kupitia wanadamu tulioumbwa na Mungu basi daima anatupotosha tumchukize aliyetuumba hivyo hata kuteka ufahamu wetu na kushindwa kujua kwamba Mungu ametupa tendo la ndoa kama zawadi na kukosa busara na kusubiri tujiandae vizuri kimaisha na kifikra kwa kuomba na kuipokea zawadi. Rai yangu ni tuzishinde hila za shetani kwa kutokubali kupumbazwa kiakili na kiroho kiasi cha kukosa mazuri yaliyo mbele yetu aliyotuahidia Baba yetu wa mbinguni kwa vitu ambayo tumeandaliwa kwa ajili yetu na kwamba kama hujapata leo una uhakika wa kuipata maana ni kwa ajili ya kila mmoja. Sifa kwako ee Mungu,maana sijui nimewaza nini leo ila naimani tu umenitumia kufikisha ujumbe huu kwa uliowakusudia. Ndugu mdogo A.B.Tumain