Majadiliano:Rasi ya Italia

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Italia peninsula - rasi[hariri chanzo]

Riccardo alitumia neno "peninsula". Sina uhakika kama neno "peninsula" limeshapokelewa katika Kiswahili. Naikumbuka kwa redio China (huduma ya Kiswahili). Lakini menginevyo nimekuta mara kwa mara "rasi" linalotaja maeneo makubwa (rasi ya Italia, rasi ya Iberia, rasi ya Korea) au sehemu ndogo kama vile Rasi ya Tumaini Jema. Lakini sipati nafasi ya kusoma ya kusoma magazeti ya Kiswahili hapa nilipo. Naomba tu kama neno (jinsi ulivyofanya katika makala Vatikani) ni vema kuangalia kama tuanyo tayari matumizi hapa kwenye wikipedia. Kwa sasa nimetumia kwa kawaida neno "rasi" katika makala mbalimbali za kijiografia. Ukiona kuna msingi wa kutumia "peninsula" naomba utaje tushauriane. Kama ni kweli neno jipya "peninsula" basi tutumie kote? --Kipala (majadiliano) 11:17, 8 Februari 2009 (UTC)[jibu]

Bado ni kitendawili kwa upande wangu. Peninsula na Cape maana zake ni sawa? Maana nikiangalia Rasi ya Tumaini Jema kwa Kiingereza inasema Cape of Good Hope - pia kule kusini mwa Afrika nimeona makala nyingi zikiandikiwa kama, Rasi ya Kaskazini, Rasi ya Mashariki, ambazo zote kwa Kiingereza zilisema "Cape". Hiyo sio mimi, ni kwa mujibu wa makala nilizozikuta tangua awali - sasa hapa naona kuna mchanganyo wa peninsula na cape. Naomba nipewe tofauti au maana halisi ya maneno hayo! --Mwanaharakati (Longa) 13:11, 9 Februari 2009 (UTC)[jibu]