Majadiliano:Lugha za Kirumi

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kilatini[hariri chanzo]

Ndugu, nimesikitika kwamba umekata habari nilizoandika kuhusu Lugha za Kirumi. Kilatini ni mama yake: ukitaka kumuelewa mtoto, ni muhimu kutaja na kufahamu wazazi! Si mpaka utumie kiungo... Naomba urekebishe mwenyewe. Kama hupendi kwamba nimetaja Kanisa Katoliki, futa hilo tu... --Riccardo Riccioni (majadiliano) 08:45, 21 Septemba 2008 (UTC)[jibu]

Riccardo, labda afadhali ningetaja sababu zangu kwanza kwenye ukurasa wa majadiliano kabla ya kusahihisha. Lakini hata hivyo tuko huru kama nimekosa basi tusahihishe upya. Sababu zangu ni hizi:
Kwa bahati mbaya sehemu za nyongeza zako katika makala hazikusaidia kuelewa "lugha za Kirumi" vema zaidi. Ni maelezo yanayohusu lugha ya kilatini. Kuna makala ya "Kilatini" na makala hii bado ni fupi inafaa kupanushwa. Sielewi unalilia nini kuhusu kanisa katoliki; ukiweza kuonyesha jinsi gani matumizi ya Kilatini kanisani yalikuwa muhimu kwa kutokea kwa lugha za Kirumi andika tu hapa; ila tu yale uliyotaja ni kuhusu maendeleo ya Kilatini chenyewe unaikuta katika makala yake (kanisa katoliki mara tatu nisipokosei hata kama ni makala mafupi tu).
Nimeona hasa nyongeza katika sentensi ya kwanza zilileta ugumu kuelewa kicha cha habari vema. Pamoja na hayo sioni ni kweli kusema Kilatini "kilikufa mwishoni mwa milenia ya kwanza"; ungesema kama Lugha ya kwanza afadhali lakini haina mahali katika sentensi ya kwanza ya makala hii; swali jinsi gani Kilatini kilikufa au hakikufa ni jambo la kujadiliwa hasa ukikumbuka nafasi yake kubwa kama lugha ya mawasiliano iliyoandikwa na pia kuzungumzwa katika Ulaya pamoja na ufufuo wake kama Kilatini Kipya wakati wa karne za 16-18. Ila tu maswali kama haya yana nafasi ndani ya makala yake si chini ya kichwa kingine.
Nahamisha mazungumzo haya kwenda ukurasa wa majadiliano ya makala yenyewe ni mahali pake. --Kipala (majadiliano) 11:00, 21 Septemba 2008 (UTC)[jibu]