Majadiliano:Karama

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Karama imetumika kwa ajili ya kanisa tu, basi wakati kumbe hata kwenye Uislamu limetumika sana. Kwa maana ya lugha au katika Kiswahili, haileti maana ikiwa neno lipo pande zote mbili. Tazama kamusi ya TUKI inasemaje:

karama* nm [i-] 1 gracious gifts, blessings. 2 talents, endowments. (Kar)

Tena neno linatoka Kiarabu kwa upande wa Kiswahili! Tafakarini makala hii isiegemee upande wowote. Hasa Riccardo!--MwanaharakatiLonga 15:14, 10 Novemba 2010 (UTC) [jibu]

Asante kwa mchango. Je una mfano wa matumizi ya "karamu" katika mafundisho ya kiislamu? Kam ni vile tunaweza kuongeza sehemu juu ya "Karamu katika Uislamu". Ila kwa sasa sikumbuki matumizi yake vile. Lakini sijaingia sana msikitini kwa Kiswahili. Kipala (majadiliano) 16:11, 10 Novemba 2010 (UTC)[jibu]
Mzee Kipala, nimeona umetumia neno karamu hata katika makala ya mwezi mtukufu wa ramadhani. Ni matumaini yangu ya kwamba huhitaji maelezo ya ziada ikiwa tayari umetumia neno kama hilo mahali fulani!--MwanaharakatiLonga 06:51, 11 Novemba 2010 (UTC)[jibu]
Kwa maana ya makala ile ni "chakula maalumu cha sikukuu au nafasi ya pekee". Lakini hii si swali la dini fulani. Makala "Karamu" inahusu vipaji kutoka kwa Mungu. Hapa sijui mengi kuhusu matumizi atika Uislamu. Kipala (majadiliano) 21:59, 11 Novemba 2010 (UTC)[jibu]