Majadiliano:Januari

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kwa kawaida Watanzania wanasema "mwezi wa kwanza", na mara chache tu wanatumia neno "Januari". Sijui kuhusu Waswahili wa Kenya na nchi nyingine, lakini wakipendelea msemo "mwezi wa kwanza" pia, tutumie jina "mwezi wa kwanza" kwa makala hii. Marcos 17:24, 11 Aprili 2007 (UTC)[jibu]

Marcos, karibu tena kwetu!! Ni kweli ya kwamba mara nyingi miezi inahesabiwa tu: mwezi wa kwanza, wa pili, wa tatu... Lakini sidhani ya kwamba mtu atatafuta sana "mwezi wa kwanza" katika kamusi. Akiona neno "Januari" atapenda kujua maana na asili ya neno. Hata hivyo imefaa kuongeza kiungo "Mwezi wa kwanza" kama "#redirect" (nimefanya). Je, una nafasi ya kuongeza hiyo kwa kila mwezi? --Kipala 17:57, 11 Aprili 2007 (UTC)[jibu]