Majadiliano:Biblia ya Kiebrania

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ningependelea kurudisha masahihisho kadhaa yaliyofanyiwa na Riccardo.

  • Sidhani ya kwamba lugha "Biblia ya Kiebrania" inatumiwa na Wakristo tu lakini na wataalamu wengi wasio Wayahudi wenyewe.
  • Lugha inaitwa Kiebrania.
  • Swali jinsi Wakristo wanavyoangalia vitabu linajadiliwa chiniy a Agnao la Kale, labda dokezo fupi tu iwepo. Mambo ya Ebr 8 heri yasijadiliwe hapa kwa sababu hii ni hoja kwa upande wa Wakristo tu.

--Kipala (majadiliano) 18:12, 8 Juni 2008 (UTC)[jibu]

Ndugu mpendwa, nakubali kwamba "Biblia ya Kiebrania" halitumiki na Wakristo tu, lakini ukiondoa Wayahudi ambao hawalitumii, wataalamu wake ni karibu wote Wakristo. Hivyo tunaweza kuongeza neno "hasa" au kusema "wasio Wayahudi". Inawezekana kwamba Wazungu wanasema "lugha ya Kiebrania", lakini kwa uzoefu wangu Waswahili wengi hawasemi hivyo. Shida kubwa kuhusu suala la vitabu vya Agano la Kale nik wamba mpaka sasa Wikipedia ya Kiswahili imefuata zaidi msimamo wa Kiprotestanti, kwa kuona vitabu hivyo ni 39 kama katika Tenak, kumbe Wakristo walio wengi wanakubali vitabu vingi zaidi, walau 7. Naomba mambo yawekwe sawa, kwa mfano katika ile lebo ya vitabu vya Agano la Kale iliyowekwa chini ya makala nyingi. Naomba ndani yake viongezwe vitabu vya Deuterokanoni kama vilivyowekwa katika Biblia Habari Njema na tafsiri nyingine za pamoja duniani: inawezekana kuvitaja peke yake kama nyongeza. Asante kwa ushirikiano. Riccardo Riccioni15:38, 9 Juni 2008 (UTC)15:38, 9 Juni 2008 (UTC)

Riccardo, nakubali kabisa kuhusu maelezo ya kidhehebu. Hapa ni baraka kwa ajili ya makala juu ya Ukristo ya kwamba wewe ukiwa mkatoliki umejiunga na wikipedia hii. Nitarekebisha maelezo juu ya idadi ya vitabu vya Agano la Kale utanisamehe nikiwa Mlutheri. Kwa jumla naona ni wazo zuri tufuate kawaida ya toleo la "Habari Njema" kwa sababu tafsiri hii ilikubaliwa katiy a madhehebu mbalimbali. Nimejitahidi (sijui kama nimefaulu?) kwa mfano nikitumia lugha ya "Roma" badala ya "Rumi" jinsi ilivyo kawaida katika Biblia ya Union Version.
Nikisema hivyo naona haja ya kutazamiana na kusaidiana. Nimeona katika makala juu ya Uislamu ya kwamba waandisha Waislamu wamependa kutumia matamshi ya heshima kama vile "(SAW)"; au pia mwandishi mkatoliki katika makala juu ya Mtaguso wa pili wa Vatikani alimtaja Papa kama "papa mwenye heri Yohane XXIII". Hii ni lugha ya heshima iliyo kawaida ndani ya kanisa hili lenyewe lakini halisaidii kueleweka kwa makala kwa mtu asiye mkatoliki; vilevile kuhusu ile "SAW" kati ya Waislamu. Kwa jumla Kiswahili cha Kidhehebu ni tatizo na tutaendelea kuliona tena na tena. Kwa bahati nzuri nilijua kuna tofauti nilipoandika makala ya "Baba yetu" lakini naomba uangalie kama umbo la kikatoliki lilikuwa sawa!
Kingine ni lile la "Kiyahudi" au "Kiebrania". Kuna uwezekano ya kwamba hata hapa kuna uzoefu wa kidhehebu. Ila tu nichungulia katika google maneno "lugha ya Kiebrania" na "lugha ya Kiyahudi" naona kurasa nyingi kabisa upande wa Kiebrania ni chache sana upande wa Kiyahudi. Tena tukiendelea kuongeza makala juu ya lugha tutapata lugha mbalimbali za "Kiyahudi" kama vile Kiyidish, Kiladino na nyingine ambazo zote zinajadiliwa na Wayahudi tu katika sehemu mbalimbali za dunia. Hadi sasa naona heri tutumie "Kiyahudi" kwa upande wa kidini na "Ebrania" kwa upande wa lugha; Unaonaje? --Kipala (majadiliano) 15:52, 10 Juni 2008 (UTC)[jibu]
Nyongeza: Naomba usaidie kuonyesha ni wapi ya kwamba makala juu ya Biblia zinahitaji masahihisho. Makala ya Agano la Kale inaonyesha tofauti katika hesabu. Je unaona nyongeza? Labda makala nyingine? --Kipala (majadiliano) 16:02, 10 Juni 2008 (UTC)[jibu]

Ndugu, asante kwa maneno yako mazuri ya kiekumeni. Nakubali tutumie "lugha ya Kiebrania". labda ni sahihi zaidi, ingawa kwa mang'amuzi yangu nikisema "ya Kiyahudi" wananielewa zaidi, kama nilivyothibitisha jana wakati wa kufundisha Divinity. Nikiona tatizo la kimadhehebu katika makala yoyote nitarekebisha kwa mtazamo wa kiekumeni. Nikishindwa kuwa neutral, mnaweza kurekebisha bila ya wasiwasi. Shalom! Riccardo Riccioni11:41, 12 Juni 2008 (UTC)11:41, 12 Juni 2008 (UTC)11:41, 12 Juni 2008 (UTC)~~