Majadiliano:Basilika la Mt. Petro

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kanisa au Kanisa Kuu?[hariri chanzo]

Kanisa la Vatikano si Kanisa kuu, ni Basilika tu: kanisa kuu la Roma ni lile la Mt. Yohane huko Laterano. Mimi ni mwenyeji wa huko. Asante tena kwa bidii zako. Amani kwako. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:28, 22 Juni 2008 (UTC) (imehamishwa kutoka User talk:Kipala)[jibu]

Asante kwa mchango huu. Sasa nimetumia "kanisa kuu" kwa neno lile la "cathedral" - je wewe umezoea neno gani? Kamusi za TUKI zatumia "kanisa kuu la dayosisi". Legere inatumia "kanisa kuu". Sijaona kosa lakini naomba useme ni nini inayoeleweka vema zaidi. Nilikumbuka ifuatayo: Zamani kwa Kilatini "Cathedralis Ecclesia" iliitwa pia "ecclesia maior"; machoni pangu hii inalingana vizuri na "kanisa kuu" nikafikiri hii ni sababu ya kwamba inaonekana hivyo katika kamusi.
Najua pia ya kwamba kwa huko Roma jina la "Basilica maior" ni kawaida. Hapo nilisita kwa sababu kwanza sikujisikia kuanzisha makala kama "basilica maior" kwa ajili ya majengo haya machache lakini sina neno ukitaka kufanya hivyo baadaye tungebadilisha makala kuwa "Basilika ya Mt. Petro" (pamoja na kusahihisha viungo). "Basilika" yenyewe ningependelea kuweka kando kwa matumizi iliyo kawaida zaidi yaani aina ya jengo la kanisa inayoitwa "basilika".
Labda useme kwanza wewe unaona neno gani kwa "cathedral" ni afadhali? Je kuna "katedrali" kwa Kiswahili?? Hadi wakati ule nitarudisha kwa sasa kiungo katika "Vatikani" kulingana na jina la makala hii hadi tupate jina tofauti. --Kipala (majadiliano) 14:27, 22 Juni 2008 (UTC)[jibu]
Nyongeza: Nimeona sasa orodha hii ya Kiitalia-Kiswahili-Kiingereza-Kilatini inaonekana ni sehemu ya kamusi yenye uzito upande wa habari za kikanisa. Nimeihifadhi kwenye tarakilishi yangu. Je unaijua? Hii inashika maneno haya yote kama katedrali na basilika. --Kipala (majadiliano) 14:45, 22 Juni 2008 (UTC)[jibu]
Hongera kwa uekumeni wako. Hiyo kamusi naijua, imetengenezwa na rafiki yangu. Lakini sikubali mapendekezo yake yote... Kwa mfano, hakuna sababu ya kutumia neno la mkopo katedrali, wakati wote wanatumia jina sahihi kabisa la Kiswahili: Kanisa Kuu. Nilichosema ni kwamba jimbo la Roma lina Kanisa kuu kama majimbo yote, ila si lile la Mt. Petro huko Vatikano, bali lile la Mt. Yohane huko Laterano. Ndiyo sababu humo ndimo yanamotunzwa mafuvu ya vichwa yanayosadikiwa kuwa ya Petro na Paulo. Hasa ndiyo sababu karibu nalo pana batizio kuu na seminari kuu ya jimbo. Mbele ya Kanisa hilo limeandikwa wazi katika marumaru: Ecclesia mater et caput ecclesiarum omnium urbis et orbis. Asante. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:53, 27 Juni 2008 (UTC)[jibu]
Sijui unataka niongeze nini zaidi kuhusu suala hili. Jimbo la Roma lina kanisa kuu huko Laterano. Askofu wa Roma anakwenda kukalia ukulu wake huko. Lile la Mt. Petro ni kubwa zaidi, linajulikana zaidi, lakini ni Basilika tu. Naomba tusogeze ukurasa huo kwenye kichwa "Kanisa la Mt. Petro Roma" --Riccardo Riccioni (majadiliano) 18:44, 10 Oktoba 2008 (UTC)[jibu]

au: "Kanisa la Mt. Petro Vatikano" --Riccardo Riccioni (majadiliano) 18:45, 10 Oktoba 2008 (UTC)[jibu]