Madende
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Madende | ||||||||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Madende ni ndege wa jenasi Cichladusa katika familia ya Muscicapidae. Zamani waliainishwa katika familia ya mikesha (Turdidae). Wana mnasaba na kurumbiza na wanafanana nao. Wana rangi ya kahawa mgongoni na nyeupe chini; madende madoadoa ana madoa meusi kidarini na tumboni. Hawa ni ndege wa misitu mikavu ya Afrika. Madume ya spishi hizi waimba vizuri. Hula wadudu hasa. Hujenga tago lao kwa umbo wa kikombe katika au chini ya kichaka. Jike huyataga mayai 2-4.
[hariri] Spishi
- Cichladusa arquata, Madende Mkufu (Collared Palm-thrush)
- Cichladusa guttata, Madende Madoadoa (Spotted Morning Thrush)
- Cichladusa ruficauda, Madende Mkia-mwekundu (Rufous-tailed Palm-thrush)