Lushoto (mji)
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Lushoto | |
| Mahali pa mji wa Lushoto katika Tanzania | |
| Anwani ya kijiografia: 4°46′48″S 38°16′48″E / 4.78°S 38.28°E | |
| Nchi | Tanzania |
|---|---|
| Mkoa | Tanga |
| Wilaya | Lushoto |
Lushoto ni mji mdogo uliopo kwa kimo cha mita 1930 juu ya UB kwenye milima ya Usambara ni makao makuu ya wilaya ya Lushoto. Mji ulianzishwa kwa jina la Wilhelmstal ("bonde la Wilhelm") na Wajerumani wakati wa koloni ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Jina lilichaguliwa kwa heshima ya kaisari Wilhelm II aliyekuwa mtawala wa Ujerumani hadi 1918.
Kuna barabara ya lami kati ya Lushoto na Mombo inapounganika na barabara kuu B1 Arusha - Dar es Salaam.
Mazingira ya Lushoto inafaa kwa kilimo kuna vivutio vya utalii pia.
Viungo vya Nje [hariri]
| Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tanga bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Lushoto (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |