Ludoviko wa Casoria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ludoviko wa Casoria, O.F.M. (Casoria, karibu na Napoli, 11 Machi 1814Posillipo, Napoli 30 Machi 1885), alikuwa mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo na padri wa Kanisa Katoliki nchini Italia.

Alipata umaarufu kwa upendo mkubwa kwa maskini uliomfanya apambane na ufukara wa jamii na kwa kuanzisha mashirika mawili ya kitawa: Ndugu wa Kijivu wa Upendo na Masista wa Kijivu wa Mt. Elizabeti.

Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri mwaka 1993[1], halafu Papa Fransisko alimtangaza mtakatifu tarehe 23 Novemba 2014.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. "The Papacy of John Paul II". Freecatholicpamphlets.org. Iliwekwa mnamo 2013-04-25. [dead link]
  2. Martyrologium Romanum

Vyanzo[hariri | hariri chanzo]

  • Acta Ordinis Minorum (May, 1907), 156-158;
  • The Catholic World (November, 1895), 155-166;
  • Voce di Sant' Antonio (July, 1907), 23-26.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.