Likokona

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Likokona ni kata ya Wilaya ya Nanyumbu katika Mkoa wa Mtwara, Tanzania, yenye postikodi namba 63607.

Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2022, kata ilikuwa na wakazi wapatao 14,707 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 18,629 waishio humo.[2]

Historia[hariri | hariri chanzo]

Kijiji cha Likokona kilianzishwa na Wamachemba waliotokea Lukumbi, eneo lililo kaskazini mwa kijiji cha Likokona cha sasa kwenye njia ya kuelekea Mwambo. Wamachemba hao, wakiongozwa na mwenye Machemba, walivuka mto Ruvuma wakitokea Msumbiji na kwa heshima ya Mwenye Machemba aliyekuwa maarufu na rafiki wa Waarabu waliomba utawala wa kikoloni mnamo mwaka 1947 wapewe eneo la kuishi. Wakati huo eneo lote la kuanzia Masasi hadi Lumesule lilikuwa hifadhi ya wanyama ambapo shughuli zozote za kibinadamu hazijuruhusiwa. Lakini kwa namna ya kushangaza Wamachemba walipewa kwenda kuishi eneo la Lukumbi lililo kaskazini mwa eneo la Likokona lenye wanyama wengi.

Baada ya hali ya maisha kutokuwa njema huko Lukumbi Wamachemba waliomba utawala wa kikoloni waondoke Lukumbi na kuelekea eneo linalojulikana kwa sasa kama Cheleweni lililo kati ya mto Lukwika na mto Likokona. Hapo waliweka kambi na kuwa na mji uliostawi sana wakati huo. Kwenye eneo hilo palikuwa na ofisi za serikali ya mkoloni na mahakama ambayo wakati huo ilifahamika kama baraza.

Baadaye wakazi wake wengi wakahamia Likokona ya sasa iliyokuwa ikiitwa Mchungwani na kuacha mji huo wa zamani ukimilikiwa na Hassan Salimu - mwenyeji wa Lindi aliyekuja kuwekeza Likokona.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Kata za Wilaya ya Nanyumbu - Mkoa wa Mtwara - Tanzania

Chipuputa | Kamundi | Kilimanihewa | Likokona | Lumesule | Mangaka | Maratani | Masuguru | Michiga | Mikangaula | Mkonona | Mnanje | Nandete | Nangomba | Nanyumbu | Napacho | Sengenya


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mtwara bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Likokona kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.