Leo Tolstoy
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lev Nikolayevich Tolstoy (Kirusi Лев Николаевич Толстой; 9 Septemba 1828-20 Novemba 1910) alikuwa mwandishi kutoka nchi ya Urusi. Huhesabiwa kati ya wanariwaya wakubwa wa fasihi ya dunia na kati ya masimulizi yake makuu ni Vita na Amani pamoja na Anna Karenina.
[hariri] Familia na urithi
Tolstoy alizaliwa katika familia ya makabaila kwenye kijiji cha Yasnaya Polyana karibu na mji Tula. Familia yake ilikuwa na uhusiano wa kindugu na makabaila wengi na Aleksander Pushkin alikuwa binamu yake.
Mapema Tolstoy alikuwa yatima baada ya kifo cha wazazi wake akalelewa na dada yake mkubwa. Alianza kusoma lugha za Kiasia halafu sheria lakini alipofikia umri wa miaka 20 aliacha masomo akaenda kuishi kwenye mashamba ya familia yake. Hapo alijikuta kama bwana wa familia za wakulima maskini aliokuwa aliwarithi kama sehemu ya mali yake wakiwa kama nusu watumwa jinsi iliovyokuwa kawaida kwa wakulima wengi wa Urusi wa siku zile kumbe akajitahidi kuboresha maisha yao..
[hariri] Mwanajeshi, mpenda amani, mla mboga
Kama mwanajeshi alishiriki katika vita za Urusi kwenye Kaukazi na vita ya Krimea. Alirudi kwake kama adui wa vita akaendelea kulaumu vita na mabavu kati ya watu akijenga imani yake kwenye mfano wa Yesu Mkristo. Imani hii ilileta baadaye ugomvi na kanisa rasmi la Urusi lililotumia imani ya Kikristo kwa kubariki jeshi la taifa wakati Tolstoy alikataa kushiriki vitani tena. Aliendelea kukataa kila aina ya kuua kwa hiyo alikataa kuchinja wanyama na kula nyama. Aliandika:
-
- Kula nyama ni mabaki ya unyama ndani ya binadamu. Ulaji mboga ni hatua ya kwanza kwenye njia ya mwangaza.
- Ni hatua moja tu kutoka uuaji wa wanyama kwenda uuaji wa wanadamu vilevile kutoka kutesa wanyama kwenda kutesa watu.
- Kama huwezi kuua watu - vizuri! Kama huwezi kuua mifugo au ndege - bora; wala samaki wala wadudu - bora tena! Ujitahidi kusogea mbele usipoteze muda kutafakari ni nini inayowezekana au haiwezekani. Fanya unachoweza.
[hariri] Ndoa na kazi ya fasihi
1862 alimwoa Sofia Andreevna Bers akazaa naye watoto 13. Kutokana na vitabu vyake juu ya vita ya Krimea alikuwa maarufu nchini Urusi na riwaya za kubwa zilizoafata zilijenga sifa zake za kimataifa.
Pamoja na riwaya aliandika pia maandiko ya kidini. Kitabu "Ufalme wa Mungu umo ndani yenu" kiliathiri watu wengi pamoja na Mahatma Gandhi na Martin Luther King.
Mwaka 1910 aliua kutokana na kifua kikuu akiwa na umri wa miaka 82.