Ladysmith Black Mambazo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ladysmith Black Mambazo

Ladysmith Black Mambazo ni kundi la muziki ambalo linaimba bila kutumia ala za muziki. Kundi hili lipo Afrika ya Kusini. Neno "Mambazo" linamaanisha "shoka" kwa Kizulu. Na "Ladysmith" ni kitongoji katika jimbo la Natal alichotoka Joseph Shabalala kiongozi na mwanzilishi wa kundi hili.

Ladysmith Black Mambazo lina albamu zaidi ya 40. Kundi hili lilipata umaarufu mkubwa liliposhirikiana na mwanamuziki wa Marekani Paul Simon kutoa albamu ya Graceland ambayo iliwashirikisha pia wanamuziki maarufu duniani kama Miriam Makeba na Hugh Masekela.

Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani wa Afrika bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ladysmith Black Mambazo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.