Lady Jay Dee

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lady Jay Dee
Jide akiwa katika pozi
Jide akiwa katika pozi
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Judith Daines Wambura Mbibo
Pia anajulikana kama Binti Machozi
Komandoo
Jidee
Jay Dee
Amezaliwa 6 Juni 1979 (1979-06-06) (umri 44)
Asili yake Mkurya
Aina ya muziki R&B
Bongo Flava
Afro-Pop
Kazi yake Mwanamuziki
Ala Sauti
Miaka ya kazi 1999-hadi leo
Studio MJ Records
FM Studio
Bakunde Production
Ame/Wameshirikiana na Mr. II
Professor Jay
Juma Nature
Inspector Haroun
Q. Chillah
Mwana FA

Judith Daines Wambura Mbibo (anafahamika zaidi kwa jina la kisanii kama Lady Jay Dee; amezaliwa mkoani Shinyanga 15 Juni 1979) ni mwanamuziki wa Bongo Flava-Afro pop kutoka nchini Tanzania[1].

Maisha ya awali

Judith Wambura alizaliwa na Martha na Lameck Isambua Mbibo ambao ndio wazazi wake. Alianza kuimba akiwa na umri wa miaka saba. Alianzia kuimba kanisani kama ilivyo kwa wasanii wengi. Baada ya kumaliza shule, Lady Jaydee aliwahi kufanya kazi Clouds FM kabla ya kuamua kujiingiza kwenye masuala ya muziki hapo mnamo miaka ya 2000.[2]

Shughuli za muziki

Alianza kujibebea heshima katika medani ya muziki kunako mwaka wa 2000 baada ya kutoa albamu yake ya kwanza iliyokwenda kwa jina la "Machozi" na kutoa single kadhaa kutoka katika albamu hiyo na kumfanya kuwa mwanamama wa kwanza katika bongo flava kwa kutumia gharama kubwa ya ujenzi wa albamu katika historia ya muziki wa kizazi kipya.

Lady Jay Dee ni msanii mwenye kumiliki studio yake mwenyewe ya kurekodia. Studio inakwenda kwa jina la Jag Records.

Jay Dee, alishawahi kuchaguliwa kuwa Mwanamuziki Bora wa Kike wa Tanzania kwa muziki wa R&B mnamo 2002, na kutumbuiza katika Kora All Africa Designers Competition, na kutuzwa "Albamu Bora ya R&B" katika Tuzo za Muziki Tanzania kunako tar. 6 Agosti 2004. Kunako mwezi wa Julai 2005, ameshinda tuzo ya "video bora ya msanii wa kike kwa Afrika Kusini".

Muziki

Albamu zake

Jay Dee, ametoa albamu saba za muziki[3]:

Marejeo

Viungo vya Nje

Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani wa Afrika bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lady Jay Dee kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.