Kyebitembe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kyebitembe ni kata ya Wilaya ya Muleba katika Mkoa wa Kagera, Tanzania yenye postikodi namba 35529 [1].

Kata hiyo imepakana na ziwa Burigi. Pia hifadhi ya Hifadhi ya Burigi-Chato inapatikana ndani ya kata. Ni mwendo wa saa 3.5 kwa usafiri wa Hiace kutoka kata ya Kyebitembe mpaka stendi ya mkoa iliyo ndani ya Manispaa ya mji wa Bukoba.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 32,349 [2]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 25,460 waishio humo.[3]

Ndani ya kata hiyo kuna sekondari moja ambayo ni Shule ya Sekondari Kanyeranyere na shule 8 za msingi ambazo ni Nyamilanda, Kanyeranyere, Kabungo, Kyebitembe, Kyabishagao, Nyanjubi, Kagasha na Kasindaga.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-08-05. Iliwekwa mnamo 2018-02-01. 
  2. https://www.nbs.go.tz, uk 172
  3. Sensa ya 2012, Kagera - Muleba-District-Council
Kata za Wilaya ya Muleba - Mkoa wa Kagera - Tanzania

Biirabo | Bisheke | Buganguzi | Buhangaza | Bulyakashaju | Bumbire | Bureza | Burungura | Goziba | Gwanseli | Ibuga | Ijumbi | Ikondo | Ikuza | Izigo | Kabirizi | Kagoma | Kamachumu | Karambi | Kasharunga | Kashasha | Katoke | Kerebe | Kibanga | Kikuku | Kimwani | Kishanda | Kyebitembe | Mafumbo | Magata Karutanga | Mayondwe | Mazinga | Mubunda | Muhutwe | Muleba | Mushabago | Ngenge | Nshamba | Nyakabango | Nyakatanga | Ruhanga | Rulanda | Rutoro


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kagera bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kyebitembe kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.