Kuwekuwe
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Kuwekuwe | ||||||||||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
|
Kuwekuwe ni ndege wadogo wa jenasi Nicator ambao wanatokea Afrika kusini kwa Sahara tu. Sikuhizi ndege hawa wanaainishwa katika familia Pycnonotidae lakini zamani wataalamu walifikiri kuwekuwe ni aina za mbwigu (Laniidae). Afadhali wapatiwe familia yao yenyewe. Ndege hawa wanafanana na korogoto na wana rangi ya zaituni juu na nyeupe au kijivu chini. Wanatofautiana na korogoto kwa madoa meupe au njano mbawani. Chakula chao ni kama kile cha mbwigu: wadudu wakubwa na mijusi midogo. Tago lao hujengwa mtini na jike huyataga mayai 2-3.
Spishi [hariri]
- Nicator chloris, Kuwekuwe Kijani (Western Nicator)
- Nicator gularis, Kuwekuwe Koo-jeupe (Eastern Nicator)
- Nicator vireo, Kuwekuwe Koo-njano (Yellow-throated Nicator)