Kundi la Halkojeni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Halkojeni

Halkojeni ni elementi sita za kundi la 16 katika mfumo radidia au jedwali ya elementi.

[hariri] Tabia za pamoja

Jina latokana na maneno mawili ya Kigiriki („Χαλκός“ = shaba, mtapo + „γεννώ“ = kuzaa, kufanya) na lamaanisha "fanya mtapo". Hii imetaja tabia ya kumenyuka haraka na metali hivyo kuunda kampaundi za kimetali. Halkojeni zote zina elektroni sita katika mizingo elektroni wa nje. Tabia hii huzisaabisha kutafuta elektroni mbili za nyongeza kuwa hali tahibi ya elektroni nane kwenye mzingo wa nje na kuwa ioni ya chaji hasi thabiti.

[hariri] Elementi

Elementi hizi ni pamoja na oksijeni (O), kibiriti (S), seleni (Se), teluri (Te), poloni (Po) na elementi sintetiki ya ununheksi (Uuh).

O na S ni simetali, Po, Se na Te ni metaolidi na nusuvipitisho, lakini Se na Te vina pia umbo ambako huitwa metali tu. Uuh imetengenezwa mara mbili tu katika maabara kwa muda usiofika hata sekunde. ar:مجموعة كالكوجين ast:Elementos del grupu 16 bg:Халкоген bs:Halkogeni elementi ca:Calcogen cs:Chalkogen de:Chalkogene en:Chalcogen eo:Elemento de grupo 16 es:Anfígeno eu:Anfigeno fi:Happiryhmä fr:Chalcogène it:Elementi del gruppo 16 ja:第16族元素 ko:16족 원소 la:Chalcogenica lmo:Calcògen lv:Halkogēni ms:Kumpulan kalkogen nds:Chalkogen nl:Zuurstofgroep nn:Chalkogen pl:Tlenowce pt:Calcogênio qu:Ch'uqichaq ru:Халькогены sh:16. grupa hemijskih elemenata sk:Chalkogény sl:Halkogen sr:16. група хемијских елемената sv:Syregruppen th:แชลโคเจน tr:Kalkojen vi:Nhóm nguyên tố 16 zh:氧族元素