| Kucha |

|
| Uainishaji wa kisayansi |
| Himaya: |
Animalia (Wanyama)
|
| Faila: |
Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
|
| Nusufaila: |
Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
|
| Ngeli: |
Aves (Ndege)
|
| Oda: |
Passeriformes (Ndege kama shomoro)
|
| Familia ya juu: |
Sylvioidea (Ndege kama kucha)
|
| Familia: |
Sylviidae (Ndege walio na mnasaba na kucha)
|
| Jenasi: |
Chamaea Gambel, 1847
Chleuasicus Blyth, 1845
Chlorornis Reichenbach, 1850
Chrysomma Blyth, 1843
Conostoma Hodgson, 1842
Fulvetta David & Oustalet, 1877
Horizorhinus Oberholser, 1899
Lioparus Oates, 1889
Lioptilus Bonaparte, 1850
Moupinia David & Oustalet, 1877
Myzornis Blyth, 1843
Neosuthora Hellmayr, 1911
Paradoxornis Gould, 1836
Psittiparus Hellmayr, 1903
Parophasma Reichenow, 1905
Pseudoalcippe Bannerman, 1923
Rhopophilus Giglioli & Salvadori, 1870
Sinosuthora Penhallurick & Robson, 2009
Suthora Hodgson, 1838
Sylvia Scopoli, 1769
|
| Spishi: |
Angalia katiba.
|
|
Kucha ni ndege wadogo wa familia Sylviidae. Wanafanana na shoro, kuchanyika na kuchamsitu, na zamani wote waliainishwa pamoja katika Sylviidae. Zamani kucha wa Afrika kusini kwa Sahara waliainishwa katika jenasi Parisoma lakini sasa wamewekwa katika jenasi Sylvia. Pengine jenasi Conostoma, Paradoxornis na jenasi nyingine za madomo-kasuku ziainishwa katika familia Paradoxornithidae. Spishi nyingi za kucha huimba vizuri sana. Ndege hawa wana rangi ya kahawia au kijivu mgongoni na nyeupe chini. Spishi kadhaa zina rangi kali zaidi. Wanatokea kanda za halijoto ya wastani na za nusutropiki katika Afrika, Asia na Ulaya. Spishi nyingi za Sylvia za Ulaya na Asia huhamia Afrika kusini kwa Sahara wakati wa majira ya baridi. Kucha hula wadudu. Hulijenga tago lao kwa umbo wa kikombe ndani ya uoto mzito, mara nyingi karibu na ardhi. Jike huyataga mayai 3-7.
Spishi za Afrika (na Ulaya) [hariri]
- Horizorhinus dohrni, Kucha wa Principe (Dohrn's Thrush-babbler au Principe Flycatcher-babbler)
- Lioptilus nigricapillus, Kucha-kilima Utosi-mweusi (Bush Blackcap)
- Parophasma galinieri, Kucha Habeshi (Abyssinian Catbird)
- Pseudoalcippe abyssinica, Kucha-kilima wa Afrika (African Hill Babbler)
- Pseudoalcippe atriceps, Kucha-kilima wa Ruwenzori (Ruwenzori Hill Babbler)
- Sylvia atricapilla, Kucha Utosi-mweusi (Eurasian Blackcap)
- Sylvia balearica, Kucha wa Baleara (Balearic Warbler)
- Sylvia boehmi, Kucha Koo-madoa (Banded Parisoma)
- Sylvia borin, Kucha-bustani (Garden Warbler)
- Sylvia cantillans, Kucha-mlima (Subalpine Warbler)
- Sylvia communis, Kucha Koo-jeupe Mkubwa (Common Whitethroat)
- Sylvia conspicillata, Kucha Miwani (Spectacled Warbler)
- Sylvia crassirostris, Kucha Sauti-nzuri Mashariki (Eastern Orphean Warbler)
- Sylvia curruca, Kucha Koo-jeupe Mdogo (Lesser Whitethroat)
- Sylvia deserti, Kucha-jangwa wa Afrika (African Desert Warbler)
- Sylvia deserticola, Kucha wa Tristram (Tristram's Warbler)
- Sylvia hortensis, Kucha Sauti-nzuri Magharibi (Western Orphean Warbler)
- Sylvia layardi, Kucha wa Layard (Layard's Warbler)
- Sylvia leucomelaena, Kucha Arabu (Red Sea Warbler)
- Sylvia lugens, Kucha Kahawia (Brown Parisoma)
- Sylvia melanocephala, Kucha Kichwa-cheusi (Sardinian Warbler)
- Sylvia melanothorax, Kucha wa Kupro (Cyprus Warbler)
- Sylvia moltonii, Kucha wa Moltoni (Moltoni's Warbler)
- Sylvia mystacea, Kucha wa Menetries (Menetries's Warbler)
- Sylvia nana, Kucha-jangwa wa Asia (Asian Desert Warbler)
- Sylvia nisoria, Kucha Milia (Barred Warbler)
- Sylvia rueppelli, Kucha wa Rüppell (Rüppell's Warbler)
- Sylvia sarda, Kucha wa Marmora (Marmora's Warbler)
- Sylvia subcaerulea, Kucha Tako-jekundu (Chestnut-vented Warbler)
- Sylvia undata, Kucha wa Dartford (Dartford Warbler)
Spishi za mabara mengine [hariri]
-
-
-
Black-breasted parrotbill
-
-
Vinous-throated parrotbill
-