Kristie Lu Stout
| Kristie Lu Stout | |
|---|---|
Kristie Lu Stout in Januari 2008 |
Kristie Lu Stout (amezaliwa 7 Desemba 1974) ni mwandishi na ntangazaji wa habari wa kutoka Marekani anayefanya kazi CNN International.
Wasifu [hariri]
Stout alisoma katika Shule ya Upili ya Lynbrook mjini San Jose, California, ambako alikuwa mwanachama mwanzilishi wa Lynbrook Speech and Debate Club, na vilevile alikuwa kielelezo bora kati ya vijana wenziwe.[1] Yeye alipata shahada ya kwanza na ya pili katika Uanahabari kutoka Chuo Kikuu cha Stanford, na akasomea Kichina katika Chuo Kikuu cha Tsinghua mjini Beijing. [2]
As of 2009[update]Yeye alijifungua mtoto hivi karibuni na[onesha uthibitisho] ndiye mtangazaji wa kipindi cha CNN Today, kinachoonyeshwa kila siku na kilichomfanya ashinde tuzo kutoka Asia Television Award kama Mtangazaji Bora.[3] Kabla ya hapo, aliwahi kutangaza kwenye kipindi cha CNN kinachohusisha teknolojia kiitwacho Spark, kipande chao cha kila siku "Tech Watch" , na kipindi cha Global Office . Yeye pia alikuwa akiandika "Beijing Byte" kwenye gazeti la South China Morning Post, na alikuwa mhariri wa Wired.com [2] na mwanachama mwanzilishi wa Sohu.
Stout anaishi nchini Hong Kong na ni aliolewa na wakili Seung Chong.[1]
Marejeo [hariri]
- ↑ 1.0 1.1 The Frequent Flyers' Friend. Stanford Magazine. Rudishwa juu ya 2008-08-07.
- ↑ 2.0 2.1 A Day in the Life of a Multi-Platform Journalist. ACM Ubiquity. Rudishwa juu ya 2007-03-01.
- ↑ Asian Television Awards 2006 Winners. Rudishwa juu ya 2007-09-06.
Viungo vya nje [hariri]
- Kristie Lu Stout profile at CNN.com
- Kristie Lu Stout on Twitter
- Kristie Lu Stout on Facebook
| Makala hii kuhusu mtu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kristie Lu Stout kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |