Kondoa (mji)
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Kata ya Kondoa | |
| Mahali pa Kondoa katika Tanzania | |
| Anwani ya kijiografia: 4°54′0″S 35°46′12″E / 4.9°S 35.77°E | |
| Nchi | Tanzania |
|---|---|
| Mkoa | Dodoma |
| Wilaya | Kondoa |
| Idadi ya wakazi | |
| - Mji | 21,878 |
Mji wa Kondoa ni mji mkuu wa Wilaya ya Kondoa, wilaya mojawapo ya Mkoa wa Dodoma. Kulingana na sensa ya mwaka 2002 idadi ya wakazi wa shehia ya Kondoa Mjini ilihesabiwa kuwa 21,878 [1]
Mji ulianza kama kituo cha biashara katika karne ya 19.
Msikiti wa kwanza ulijengwa mwaka 1885.
Wakati wa ukoloni wa Kijerumani mji ulijulikana kwa jina Kondoa-Irangi ukawa kituo cha jeshi la kikoloni la Kijerumani.
Mwaka 1912 ilikuwa makao makuu ya mkoa mpya wa Kondoa-Irangi.
Mwaka 1910, kanisa la kwanza lilijengwa.
Kuanzia mwaka 2011 Kondoa ni makao makuu ya jimbo jipya la Kanisa Katoliki, linaloongozwa na askofu Bernardin Mfumbusa.
Ndani ya wilaya ya Kondoa kuna vijiji zaidi ya 180.
Makabila makuu ni Warangi, Wasandawe, Waburunge na Wasi.
Marejeo [hariri]
| Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Dodoma bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kondoa (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |