Komba
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Komba | ||||||||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Komba magharibi (Galago senegalensis)
|
||||||||||||||||
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
||||||||||||||||
| Ngazi za chini | ||||||||||||||||
|
Jenasi 4: |
Komba ni wanyama wadogo wa familia Galagidae. Wamo miongoni mwa wanyama wa asili wa jamaa ya binadamu. Wanatokea Afrika kusini kwa Sahara. Hukiakia usiku na hulala mchana katika matundu ya miti. Kwa hivyo wana macho makubwa ili kuona vizuri kwa giza. Hata masikio yao ni makubwa ili kusikia mawindo yao na hata maadui yao. Mkia mrefu wao uzuia wasiyumba wakitembea juu ya matawi. Wanaweza kuruka sana, hadi m 2 kwa wima. Wana kucha kama zile za watu, isipokuwa ule wa kidole cha pili cha miguu ambao ni mrefu wenye ncha kali na hutumika kwa kusafisha manyoya. Hula wadudu, wanyama wadodo, matunda na sandarusi.
Spishi [hariri]
- Euoticus elegantulus, Komba Makucha-sindano Kusi (Southern needle-clawed bushbaby)
- Euoticus pallidus, Komba Makucha-sindano Kaskazi (Northern needle-clawed bushbaby)
- Galago gallarum, Komba Somali (Somali lesser galago)
- Galago matschiei, Komba Miwani (Spectacled lesser galago)
- Galago moholi, Komba Kusi (Southern lesser galago)
- Galago senegalensis, Komba Magharibi (Northern lesser galago)
- Galagoides cocos, Komba Mdogo wa Kenya (Kenya coast galago)
- Galagoides demidovii, Komba Mdogo wa Demidoff (Demidoff's dwarf galago)
- Galagoides granti, Komba Mdogo wa Grant (Grant's lesser galago)
- Galagoides nyasae, Komba Mdogo wa Malawi (Malawi galago)
- Galagoides orinus, Komba Mdogo wa Uluguru (Mountain dwarf galago)
- Galagoides rondoensis, Komba Mdogo wa Rondo (Rondo dwarf galago)
- Galagoides thomasi, Komba Mdogo wa Thomas (Thomas's dwarf galago)
- Galagoides zanzibaricus, Komba Mdogo wa Pwani (Coast galago)
- Galagoides z. udzungwensis, Komba Mdogo wa Udzungwa (Udzungwa galago)
- Galagoides z. zanzibaricus, Komba Mdogo wa Zanzibar (Zanzibar galago)
- Otolemur crassicaudatus, Komba-miombo (Brown greater galago)
- Otolemur garnettii, Komba Kaskazi (Northern greater galago)
- Otolemur monteiri, Komba wa Kavirondo (Silvery greater galago)