Kolo
| Kata ya Kolo | |
| Sehemu ya kata ya Kolo kutoka hewani | |
| Nchi | Tanzania |
|---|---|
| Mkoa | Dodoma |
| Wilaya | Kondoa |
| Idadi ya wakazi | |
| - Mji | 8,268 |
Kolo ni jina la kata ya Wilaya ya Kondoa katika Mkoa wa Dodoma, Tanzania. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2002, kata ina wakazi wapatao 8,268 waishio humo.[1]
Kolo iko kwenye barabara kuu kati ya Babati na Kondoa.
Baadhi ya vijiji vya kata ya Kolo vyenye shule ya msingi ni Kolo yenyewe, Bolisa, Gubali, Hachwi na Itiso. Asilimia kubwa za wakazi wa kata ya Kolo ni Warangi, ingawa zamani ilikuwa eneo la Waalagwa.
Shule ya msingi ya Kolo ilifunguliwa mwaka wa 1917 ikiwa ni shule ya kwanza katika wilaya ya Kondoa. Ilifunguliwa chini ya utawala wa Sultani Salimu Kimolo ambaye ikulu yake bado ipo katika kijiji cha Kolo.
Pia, kata ya Kolo ni maarufu kama mahali pa kufikia kwa michoro ya Kondoa kwa sababu hapa barabara kuu inafika karibu na sehemu ya michoro hii.
Marejeo [hariri]
- ↑ Ripoti Kuu ya Hesabu ya Sensa ya Watu na Makazi kwa Mwaka wa 2002 (en). Serikali ya Tanzania.
| Kata za Wilaya ya Kondoa - Mkoa wa Dodoma - Tanzania | ||
|---|---|---|
|
Bereko | Bumbuta | Busi | Chandama | Changaa | Chemba | Dalai | Farkwa | Goima | Gwandi | Haubi | Jangalo | Kalamba | Kikilo | Kikore | Kingale | Kisese | Kolo | Kondoa Mjini | Kwadelo | Kwamtoro | Lalta | Makorongo | Masange | Mnenia | Mondo | Mpendo | Mrijo | Ovada | Pahi | Paranga | Sanzawa | Soera | Suruke | Thawi |
||
| Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Dodoma bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kolo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |