Koleta Boylet
Nicolette Boylet alizaliwa Corbie (Ufaransa) tarehe 13 Januari 1381 katika familia duni.
Ni maarufu kwa kuanzisha urekebisho wa matawi mbalimbali ya Wafransisko ambao walioufuata wanaitwa kwa heshima yake Wakoleta.
Kisha kuishi utawani sehemu mbalimbali, akichukia ulegevu uliotawala huko, alijifungia upwekeni (1402-1406), halafu akakubaliwa na antipapa Benedikto XIII ruhusa ya kurekebisha na kuanzisha monasteri ili zifuate ufukara walioutaka Fransisko wa Asizi na Klara wa Asizi.
Alifariki tarehe 6 Machi 1447 huko Gand (leo Ubelgiji), katika moja ya monasteri 17 za Waklara alizozianzisha.
Alitangazwa na Papa Klementi XII kuwa mwenye heri tarehe 23 Januari 1740, halafu Papa Pius VII alimtaja kuwa mtakatifu tarehe 24 Mei 1807.
Picha [hariri]
-
Kanzu yake
Ghent, Belgium
Marejeo [hariri]
- Colette of Corbie (1381 - 1447): Learning and Holiness, Franciscan Institute Publications, 2010. ISBN 9781576592175
Viungo vya nje [hariri]
| Wikisource has original text related to this article: |