Koikoi
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Koikoi | ||||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
|
||||||||||||
| Ngazi za chini | ||||||||||||
|
Spishi 12:
|
Koikoi ni ndege wakubwa wa jenasi Ardea katika familia ya Ardeidae wenye miguu mirefu na domo refu na nyembamba. Hupinda shingo yao wakiruka angani. Ndege hawa wana rangi nyeupe, kijivu na nyeusi. Spishi zenye rangi ya kahawiachekundu huitwa pondagundi pia. Spishi nyingine nyeupe kabisa inaitwa msuka. Ilikuwa imeainishwa ndani ya jenasi Egretta mpaka juzi. Koikoi hupenda kula samaki lakini hula wanyama wadogo pia, kama vyura, mijusi na nyoka. Hujenga matago yao kwa matawi juu ya miti. Jike huyataga mayai 2-6.
Yaliyomo |
[hariri] Spishi za Afrika
- Ardea alba, Msuka (Great White Egret)
- Ardea cinerea, Koikoi Kijivu (Grey Heron)
- Ardea goliath, Pondagundi Mkubwa au Koikoi Jitu (Goliath Heron)
- Ardea humbloti, Koikoi wa Madagaska (Madagascar Heron)
- Ardea melanocephala, Koikoi Majoka (Black-headed Heron)
- Ardea purpurea, Pondagundi (Purple Heron)
[hariri] Spishi za mabara mengine
- Ardea cocoi (Cocoi Heron)
- Ardea herodias (Great Blue Heron)
- Ardea insignis (White-bellied Heron)
- Ardea pacifica (White-necked or Pacific Heron)
- Ardea picata (Pied Heron)
- Ardea sumatrana (Great-billed Heron)
[hariri] Spishi za kabla ya historia
- Ardea bennuides (Bennu Heron)
- Ardea formosa
- Ardea howardae
- Ardea polkensis (Mwanzo wa Pliocene ya Bone Valley, MMA)
- Ardea similis
- Ardea sp. (Kati ya Miocene ya Observation Quarry, MMA)
- Ardea sp. (Mwisho wa Miocene ya Love Bone Bed , MMA)
- Ardea sp. (Mwanzo wa Pleistocene ya Macasphalt Shell Pit, MMA)