Klemens wa Aleksandria
Titus Flavius Clemens (Kigiriki: Klemes Alexandreus, Κλήμης Αλεξανδρεύς ; * mnamo 150 Athens; † mnamo 215 Aleksandria) anayejulikana zaidi kama Klemens wa Alexandria alikuwa mtaalamu na mwanafalsafa Mkristo katika mji wa Aleksandria (Misri) mwanzoni wa karne ya tatu BK. Huhesabiwa kati ya walimu muhimu wa kanisa la kwanza.
Klemens alikuwa mwenyeji wa Ugiriki aliyezaliwa katika familia ya wapagani matajiri mjini Athens. Baada ya kupokea imani ya kikristo alisafiri akitembelea walimu Wakristo katika nchi mbalimbali kama vile Ugiriki, Italia na Palestina hadi Misri. Hapa alipewa nafasi ya kufundisha kwenye Chuo cha Kikristo cha Aleksandria akishirikiana na mwanzilishi wake Panteno.
Jitihada ya Klementi ilikuwa kupatanisha imani ya Kikristo na dhana za falsafa ya Kigiriki. Alifaulu kutafsiri Ukristo kwa wasomi wapagani na kuvuta wengi kwa imani mpya. Klement alikuwa mwalimu wa Origene.