Kizigula

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kizigula (pia Kizigua) ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na Wazigula. Mwaka wa 1993 idadi ya wasemaji wa Kizigula imehesabiwa kuwa watu 355,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kizigula iko katika kundi la G30.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Msamiati[hariri | hariri chanzo]

Maneno ya Kizigua na maana zake kwa Kiswahili:

  • Kizigua - kwa Kiswahili
  • Mgosi = Mwanaume
  • Mwana = Mtoto
  • Mwana wa Chigosi = Mtoto wa Kiume
  • Mwana wa Chivyele = Mtoto wa kike
  • Uta = Upinde
  • Nguku = Kuku
  • Biga = Mtungi
  • Mazi = Maji
  • Uchi = Asali
  • Sila = Barabara

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Maho, Jouni & Bonny Sands. 2002. The languages of Tanzania: a bibliography. (Orientalia et africana gothoburgensia, no 17.) Göteborg: Acta Universitatis Gothoburgensis. Pp ix, 428. ISBN 91-7346-454-6

Kitabu hiki kinataja marejeo mengine kama:

  • Dammann, Ernst. 1937/38. Zigula-Märchen. Zeitschrift für Eingeborenen-Sprachen, 28 (2), uk.139-157.
  • Kisbey, Walter H. 1896. Zigula exercises, compiled for the Universities’ Mission to Central Africa. London: Society for Promoting Christian Knowledge (SPCK). Kurasa 116.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kizigula kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.