Kitumbuka
Kitumbuka ni lugha ya Kibantu nchini Malawi inayozungumzwa na Watumbuka. Mwaka wa 2001 idadi ya wasemaji wa Kitumbuka nchini Malawi imehesabiwa kuwa watu milioni moja. Pia kuna wasemaji 142,000 nchini Zambia. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kitumbuka kiko katika kundi la N20.
Viungo vya nje [hariri]
- lugha ya Kitumbuka kwenye Multitree
- ramani ya Kitumbuka
- http://www.ethnologue.org/show_language.asp?code=tum
Viambishi ni mofimu au viungo vyenye maana ambavyo hufungamanishwa na mzizi/shina la neno ili kulipa neno hilo maana mbalimbali za kisarufi kama vile nafsi, wakati, hali, urejeshi, n.k Viambishi awali ni vile vinavyotangulia mzizi wenyewe, yaani huwa kabla ya mzizi/shina. SHINA AU MZIZI: Hakuna tofauti kati ya shina na mzizi MZIZI/SHINA, Ni sehemu ya neno inayobeba maana yake kuu na huwa haibadiliki, Kwa mfano, tuangalie vitenzi vifuatavyo: a-na-LIM-a wa-li-LIM-i-a ni-ta-LIM-iw-a wa-na-vyo-LIM-a Ukiangalia kwa makini, utaona kuna sehemu ya kitenzi hiki ambayo haibadiliki katika mifano ya hapo juu. Sehemu hiyo ni (-LIM-). Na hii ndiyo shina au mzizi wa kitenzi LIMA. Mfano mwingine: a-li-ki-SOM-a hu-SOM-ew-a wa-li-SOM-e-an-a a-li-m-SOM-e-a i-li-SOM-w-a Tunaona hapa mzizi/shina la kitenzi SOMA, ni -som- Ili utambue shina/mzizi wa kitenzi unafaa kuwazia hali mbalimbali au kauli tofautitofauti za mnyambuliko wa kitenzi halafu ubainishe sehemu isiyobadilika.