Kitamajaq
Kitamajaq (pia Kitawallammat) ni lugha ya Kiafrika-Kiasia nchini Niger na Mali inayozungumzwa na Watamajaq. Mwaka wa 1998 idadi ya wasemaji wa Kitamajaq nchini Niger imehesabiwa kuwa watu 450,000. Pia kuna wasemaji 190,000 nchini Mali na wachache wengine nchini Nigeria. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kitamajaq kiko katika kundi la Kiberber.
Viungo vya nje [hariri]
- lugha ya Kitamajaq kwenye Multitree
- ramani ya Kitamajaq
- http://www.ethnologue.org/show_language.asp?code=ttq
Viambishi ni mofimu au viungo vyenye maana ambavyo hufungamanishwa na mzizi/shina la neno ili kulipa neno hilo maana mbalimbali za kisarufi kama vile nafsi, wakati, hali, urejeshi, n.k Viambishi awali ni vile vinavyotangulia mzizi wenyewe, yaani huwa kabla ya mzizi/shina. SHINA AU MZIZI: Hakuna tofauti kati ya shina na mzizi MZIZI/SHINA, Ni sehemu ya neno inayobeba maana yake kuu na huwa haibadiliki, Kwa mfano, tuangalie vitenzi vifuatavyo: a-na-LIM-a wa-li-LIM-i-a ni-ta-LIM-iw-a wa-na-vyo-LIM-a Ukiangalia kwa makini, utaona kuna sehemu ya kitenzi hiki ambayo haibadiliki katika mifano ya hapo juu. Sehemu hiyo ni (-LIM-). Na hii ndiyo shina au mzizi wa kitenzi LIMA. Mfano mwingine: a-li-ki-SOM-a hu-SOM-ew-a wa-li-SOM-e-an-a a-li-m-SOM-e-a i-li-SOM-w-a Tunaona hapa mzizi/shina la kitenzi SOMA, ni -som- Ili utambue shina/mzizi wa kitenzi unafaa kuwazia hali mbalimbali au kauli tofautitofauti za mnyambuliko wa kitenzi halafu ubainishe sehemu isiyobadilika.