Kisimbiti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kisuba (Tanzania))

Kisimbiti (au Kisuba-Kisimbiti) ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na Wasimbiti, Wahacha, Wakine, Wasweta, Wasurwa na Waroba. Pia huitwa Kisuba-Kisimbiti. Lahaja zake ni pamoja na Kihacha, Kisweta na Kisurwa. Lugha ya Kisuba-Kisimbiti isichanganywe na lugha ya Kisuba nchini Kenya.

Mwaka wa 2011 idadi ya wasemaji wa Kisimbiti imehesabiwa kuwa watu 113,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kisimbiti iko katika kundi la E40.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Maho, Jouni & Bonny Sands. 2002. The languages of Tanzania: a bibliography. (Orientalia et africana gothoburgensia, no 17.) Göteborg: Acta Universitatis Gothoburgensis. Pp ix, 428. ISBN 91-7346-454-6
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kisimbiti kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.