Kisoo
Kisoo ni lugha ya Kinilo-Sahara nchini Uganda inayozungumzwa na Wasoo. Mwaka wa 2002 idadi ya Wasoo imehesabiwa kuwa watu 21,534 lakini idadi ya wasemaji ni wachache zaidi kwa vile ni wazee tu ambao wamebaki kuizungumza lugha hiyo; Wasoo wengi wamebadili lugha na kuongea Kikaramojong kama lugha yao. Kwa hiyo inawezekana kuwa Kisoo kitatoweka hivi naribuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kisoo kiko katika kundi la Kikuliak ambalo ni tofauti sana na lugha nyingine za Kinilo-Sahara.
Viungo vya nje[hariri]
- lugha ya Kisoo kwenye Multitree
- ramani ya Kisoo
- http://www.ethnologue.org/show_language.asp?code=teu
Viambishi ni mofimu au viungo vyenye maana ambavyo hufungamanishwa na mzizi/shina la neno ili kulipa neno hilo maana mbalimbali za kisarufi kama vile nafsi, wakati, hali, urejeshi, n.k Viambishi awali ni vile vinavyotangulia mzizi wenyewe, yaani huwa kabla ya mzizi/shina. SHINA AU MZIZI: Hakuna tofauti kati ya shina na mzizi MZIZI/SHINA, Ni sehemu ya neno inayobeba maana yake kuu na huwa haibadiliki, Kwa mfano, tuangalie vitenzi vifuatavyo: a-na-LIM-a wa-li-LIM-i-a ni-ta-LIM-iw-a wa-na-vyo-LIM-a Ukiangalia kwa makini, utaona kuna sehemu ya kitenzi hiki ambayo haibadiliki katika mifano ya hapo juu. Sehemu hiyo ni (-LIM-). Na hii ndiyo shina au mzizi wa kitenzi LIMA. Mfano mwingine: a-li-ki-SOM-a hu-SOM-ew-a wa-li-SOM-e-an-a a-li-m-SOM-e-a i-li-SOM-w-a Tunaona hapa mzizi/shina la kitenzi SOMA, ni -som- Ili utambue shina/mzizi wa kitenzi unafaa kuwazia hali mbalimbali au kauli tofautitofauti za mnyambuliko wa kitenzi halafu ubainishe sehemu isiyobadilika.