Kirangi
Kirangi ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na Warangi.
Mfumo wa Sauti (Fonolojia)[hariri]
Lugha ya Kirangi ina irabu 7 na konsonanti 22. Pia tofauti kati ya irabu fupi na irabu ndefu huleta tofauti za maana. Tena, kuna toni (au mawimbi ya sauti) zinazotofautisha maana ya nomino fulani, na nyakati za vitenzi.
Viungo vya nje[hariri]
- lugha ya Kirangi kwenye Multitree
- ramani ya Kirangi
- http://www.ethnologue.org/show_language.asp?code=lag
- http://www.african.gu.se/tanzania/weblinks.html
- http://www.linguistics.berkeley.edu/CBOLD/Docs/TLS.html (tovuti hiyo ina msamiati wa Kirangi)
Marejeo[hariri]
- Maho, Jouni & Bonny Sands. 2002. The languages of Tanzania: a bibliography. (Orientalia et africana gothoburgensia, no 17.) Göteborg: Acta Universitatis Gothoburgensis. Pp ix, 428. ISBN 91-7346-454-6
Kitabu hiki kinataja marejeo mengine kama:
- Dempwolff, Otto. 1915/16. Beiträge zur Kenntnis der Sprachen in Deutsch-Ostafrika. Teil 8: Irangi (Langi). Zeitschrift für Kolonialsprachen, 6, uk.102-123.
- Seidel, August. 1898. Grammatik der Sprache von Irangi. Katika: Die mittleren Hochländer des nördlischen Deutsch-Ostafrika, uk.387-435. Kuhaririwa na C. Waldemar Werther. Berlin: Verlag von Hermann Paetel.
Viambishi ni mofimu au viungo vyenye maana ambavyo hufungamanishwa na mzizi/shina la neno ili kulipa neno hilo maana mbalimbali za kisarufi kama vile nafsi, wakati, hali, urejeshi, n.k Viambishi awali ni vile vinavyotangulia mzizi wenyewe, yaani huwa kabla ya mzizi/shina. SHINA AU MZIZI: Hakuna tofauti kati ya shina na mzizi MZIZI/SHINA, Ni sehemu ya neno inayobeba maana yake kuu na huwa haibadiliki, Kwa mfano, tuangalie vitenzi vifuatavyo: a-na-LIM-a wa-li-LIM-i-a ni-ta-LIM-iw-a wa-na-vyo-LIM-a Ukiangalia kwa makini, utaona kuna sehemu ya kitenzi hiki ambayo haibadiliki katika mifano ya hapo juu. Sehemu hiyo ni (-LIM-). Na hii ndiyo shina au mzizi wa kitenzi LIMA. Mfano mwingine: a-li-ki-SOM-a hu-SOM-ew-a wa-li-SOM-e-an-a a-li-m-SOM-e-a i-li-SOM-w-a Tunaona hapa mzizi/shina la kitenzi SOMA, ni -som- Ili utambue shina/mzizi wa kitenzi unafaa kuwazia hali mbalimbali au kauli tofautitofauti za mnyambuliko wa kitenzi halafu ubainishe sehemu isiyobadilika.