Kiparara

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kiparara
Viparara wa Afrika
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Charadriiformes (Ndege kama vitwitwi)
Familia: Rhynchopidae (Ndege walio na mnasaba na viparara)
Jenasi: Rhynchops
Linnaeus, 1758
Spishi: Angalia katiba

Viparara (au Ndege-msumeno) ni ndege wa bahari wa jenasi Rhynchops, jenasi pekee ya familia Rhynchopidae (Rynchops na Rynchopidae ni tahajia nyingine za asili na sahihi kwa mujibu wa uainishaji). Ndege hawa wanafanana na buabua lakini wana domo ambalo sehemu yake ya chini ni refu kuliko ile ya juu. Hupuruka kwa urefu mdogo juu ya maji wakiitia sehemu ya chini ya domo lao majini ili kuwakamata samaki wadogo. Jike hutaga mayai 3-6 kwa pwani za kanda za tropiki na za karibu na tropiki.

[hariri] Spishi ya Afrika

[hariri] Spishi za mabara mengine

[hariri] Picha