Kipanga-kekeo
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Kipanga-kekeo | ||||||||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Vipanga-kekeo ni ndege mbua wa jenasi Aviceda katika familia ya Accipitridae. Ndege hawa ni vipanga wanaofanana na kekeo. Spishi zote zina kishungi. Vipanga-kekeo wanatokea misituni kwa Afrika, Asia na Australia. Hula wadudu wakubwa, Orthoptera (nzige na jamii) hasa, mijusi na nyoka, ndege na wanyama wadogo. Hujenga tago lao mtini na hutaga mayai mawili hadi matano.
[hariri] Spishi za Afrika
- Aviceda cuculoides, Kipanga-kekeo wa Afrika (African Cuckoo Hawk)
- Aviceda madagascariensis, Kipanga-kekeo wa Madagaska (Madagascar Cuckoo Hawk)
[hariri] Spishi za mabara mengine
- Aviceda jerdoni (Jerdon's Baza)
- Aviceda leuphotes (Black Baza)
- Aviceda subcristata (Pacific Baza)