Kinyanja
Kinyanja (pia Chichewa) ni lugha ya Kibantu inayozungumzwa nchini Malawi kama lugha rasmi na lugha ya taifa. Mwaka wa 2001 idadi ya wasemaji wa Kinyanja nchini Malawi imehesabiwa kuwa watu milioni saba. Pia kuna wasemaji 803,000 nchini Zambia (2001), 599,000 nchini Msumbiji (2006), na 252,000 nchini Zimbabwe (1969). Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kinyanja kiko katika kundi la N30.
Viungo vya nje [hariri]
- lugha ya Kinyanja kwenye Multitree
- ramani ya Kinyanja
- http://www.ethnologue.org/show_language.asp?code=nya
Viambishi ni mofimu au viungo vyenye maana ambavyo hufungamanishwa na mzizi/shina la neno ili kulipa neno hilo maana mbalimbali za kisarufi kama vile nafsi, wakati, hali, urejeshi, n.k Viambishi awali ni vile vinavyotangulia mzizi wenyewe, yaani huwa kabla ya mzizi/shina. SHINA AU MZIZI: Hakuna tofauti kati ya shina na mzizi MZIZI/SHINA, Ni sehemu ya neno inayobeba maana yake kuu na huwa haibadiliki, Kwa mfano, tuangalie vitenzi vifuatavyo: a-na-LIM-a wa-li-LIM-i-a ni-ta-LIM-iw-a wa-na-vyo-LIM-a Ukiangalia kwa makini, utaona kuna sehemu ya kitenzi hiki ambayo haibadiliki katika mifano ya hapo juu. Sehemu hiyo ni (-LIM-). Na hii ndiyo shina au mzizi wa kitenzi LIMA. Mfano mwingine: a-li-ki-SOM-a hu-SOM-ew-a wa-li-SOM-e-an-a a-li-m-SOM-e-a i-li-SOM-w-a Tunaona hapa mzizi/shina la kitenzi SOMA, ni -som- Ili utambue shina/mzizi wa kitenzi unafaa kuwazia hali mbalimbali au kauli tofautitofauti za mnyambuliko wa kitenzi halafu ubainishe sehemu isiyobadilika.