Kindau

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Kindau ni lugha ya Kibantu nchini Msumbiji na Zimbabwe inayozungumzwa na Wandau. Mwaka wa 2006 idadi ya wasemaji wa Kindau nchini Msumbiji imehesabiwa kuwa watu 1,580,000. Pia kuna wasemaji 800,000 nchini Zimbabwe. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kindau kiko katika kundi la S10. Kindau kinafanana sana na Kishona, na wataalamu wengine wanakiangalia kama lahaja ya Kishona tu.

Viungo vya nje [hariri]

Viambishi ni mofimu au viungo vyenye maana ambavyo hufungamanishwa na mzizi/shina la neno ili kulipa neno hilo maana mbalimbali za kisarufi kama vile nafsi, wakati, hali, urejeshi, n.k Viambishi awali ni vile vinavyotangulia mzizi wenyewe, yaani huwa kabla ya mzizi/shina. SHINA AU MZIZI: Hakuna tofauti kati ya shina na mzizi MZIZI/SHINA, Ni sehemu ya neno inayobeba maana yake kuu na huwa haibadiliki, Kwa mfano, tuangalie vitenzi vifuatavyo: a-na-LIM-a wa-li-LIM-i-a ni-ta-LIM-iw-a wa-na-vyo-LIM-a Ukiangalia kwa makini, utaona kuna sehemu ya kitenzi hiki ambayo haibadiliki katika mifano ya hapo juu. Sehemu hiyo ni (-LIM-). Na hii ndiyo shina au mzizi wa kitenzi LIMA. Mfano mwingine: a-li-ki-SOM-a hu-SOM-ew-a wa-li-SOM-e-an-a a-li-m-SOM-e-a i-li-SOM-w-a Tunaona hapa mzizi/shina la kitenzi SOMA, ni -som- Ili utambue shina/mzizi wa kitenzi unafaa kuwazia hali mbalimbali au kauli tofautitofauti za mnyambuliko wa kitenzi halafu ubainishe sehemu isiyobadilika.