Kinampanda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Kata ya Kinampanda
Nchi Tanzania
Mkoa Singida
Wilaya Iramba
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 11,030

Kinampanda ni kata ya Wilaya ya Iramba katika Mkoa wa Singida, Tanzania, yenye msimbo wa posta 43302.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 11,030 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 14,870 waishio humo.[2]

Historia[hariri | hariri chanzo]

Jina la kata linatokana na kijiji cha Kinampanda (sasa Kyalosangi) ambapo Wanyiramba wa ukoo wa Kinampanda wanaishi, yaani ni eneo la Wanampanda (ukoo). Hili ni eneo pembeni mwa kingo za milima tofali ya Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki linaloanzia maeneo ya Iguguno kuekea kaskazini ambako Mkoa wa Singida unapakana na Mikoa ya Arusha na Simiyu.

Wamisionari wa kwanza wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri walifika Uwanza (mojawapo ya vijiji vya kata ya Kinampanda) miaka ya 1930 na kujenga kanisa hapo. Baadaye, kutokana na mvutano na watu wa dini nyingine, na kuvutiwa na hali ya hewa inayotokana na kuwa juu ya Bonde la Ufa, waliamua kuhamishia makazi yao huko na kujenga kanisa kubwa mwaka 1945 ambalo lilikarabatiwa mwaka 1990.

Kinampanda ni mojawapo ya eneo maarufu mkoani Singida. Ndipo taasisi za kwanza za elimu zilipojengwa na kuzalisha wasomi lukuki. Kinampanda Middle School ilianza miaka ya 1940, ikafuatiwa na Shule ya Sekondari Tumaini miaka ya 1960 na Chuo cha Ualimu Kinampanda miaka ya 1970 vilivyoanzishwa na Kanisa la Kiinjili, Sinodi ya Kati (sasa Dayosisi ya Kati) na baadaye kutaifishwa na serikali miaka ya 1970.

Walimu waliokuwa wakifundisha Kinampanda Middle School, walishirikiana na wazalendo wengine na walianzisha tawi la TANU la kwanza mkoani Singida na kuanza harakati za kudai uhuru. Kati ya waanzilishi hao wapo Mwalimu David Nkurlu, Levy Shankala, Nagunwa Lyuki, Mohamed Masamaki na Jackson Kasuwi.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Kata za Wilaya ya Iramba - Mkoa wa Singida - Tanzania

Kaselya | Kidaru | Kinampanda | Kiomboi | Kisiriri | Kyengege | Maluga | Mbelekese | Mgongo | Mtekente | Mtoa | Mukulu | Ndago | Ndulungu | Ntwike | Old-Kiomboi | Shelui | Tulya | Ulemo | Urughu


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Singida bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kinampanda kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.