Kimurle

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kimurle ni lugha ya Kinilo-Sahara nchini Sudan Kusini inayozungumzwa na Wamurle. Mwaka wa 1982 idadi ya wasemaji wa Kimurle nchini Sudan Kusini imehesabiwa kuwa watu 60,000. Pia kulikuwa wasemaji nchini Ethiopia lakini katika sensa ya 2007, miongoni mwa Wamurle 970, mmoja tu alidai kuongea Kimurle. Inawezekana kuwa lugha ya Kimurle imekaribia kutoweka nchini Ethiopia lakini nchini Sudan Kusini inaendelea kutumiwa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kimurle iko katika kundi la Kisurmi.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kimurle kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.