Kimbandja
Kimbandja ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inayozungumzwa na Wambandja. Idadi ya wasemaji wa Kimbandja nchini Kongo imehesabiwa kuwa watu 352,000. Pia kuna wasemaji 10,460 nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati na 9060 nchini Jamhuri ya Kongo. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kimbandja kiko katika kundi la Kiadamawa-Ubangi.
Viungo vya nje [hariri]
- lugha ya Kimbandja kwenye Multitree
- ramani ya Kimbandja
- http://www.ethnologue.org/show_language.asp?code=zmz
Viambishi ni mofimu au viungo vyenye maana ambavyo hufungamanishwa na mzizi/shina la neno ili kulipa neno hilo maana mbalimbali za kisarufi kama vile nafsi, wakati, hali, urejeshi, n.k Viambishi awali ni vile vinavyotangulia mzizi wenyewe, yaani huwa kabla ya mzizi/shina. SHINA AU MZIZI: Hakuna tofauti kati ya shina na mzizi MZIZI/SHINA, Ni sehemu ya neno inayobeba maana yake kuu na huwa haibadiliki, Kwa mfano, tuangalie vitenzi vifuatavyo: a-na-LIM-a wa-li-LIM-i-a ni-ta-LIM-iw-a wa-na-vyo-LIM-a Ukiangalia kwa makini, utaona kuna sehemu ya kitenzi hiki ambayo haibadiliki katika mifano ya hapo juu. Sehemu hiyo ni (-LIM-). Na hii ndiyo shina au mzizi wa kitenzi LIMA. Mfano mwingine: a-li-ki-SOM-a hu-SOM-ew-a wa-li-SOM-e-an-a a-li-m-SOM-e-a i-li-SOM-w-a Tunaona hapa mzizi/shina la kitenzi SOMA, ni -som- Ili utambue shina/mzizi wa kitenzi unafaa kuwazia hali mbalimbali au kauli tofautitofauti za mnyambuliko wa kitenzi halafu ubainishe sehemu isiyobadilika.