Kimalagasy Sanifu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kimalagasy Sanifu (pia Kimalagasy cha Juu) ni lugha ya Kiaustronesia nchini Madagaska inayozungumzwa na Wamalagasy; tena ndiyo lugha rasmi ya Madagaska. Kufuatana na uainishaji wa lugha wa ndani zaidi, Kimalagasy Sanifu iko katika kundi la Kibarito.

Mwaka wa 2006 idadi ya wasemaji wa Kimalagasy Sanifu ilihesabiwa kuwa 7,520,000. Pia kuna wasemaji 8000 nchini Reunion na 700 nchini Komori.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kimalagasy Sanifu kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.