Kimakonde
Kimakonde ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania na Msumbiji inayozungumzwa na Wamakonde. Mwaka wa 2006 idadi ya wasemaji wa Kimakonde nchini Tanzania imehesabiwa kuwa watu 960,000. Pia kuna wasemaji 360,000 nchini Msumbiji. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kimakonde kiko katika kundi la P20.
Viungo vya nje [hariri]
- lugha ya Kimakonde kwenye Multitree
- ramani ya Kimakonde
- http://www.ethnologue.org/show_language.asp?code=kde
- http://www.african.gu.se/tanzania/weblinks.html
- http://www.linguistics.berkeley.edu/CBOLD/Docs/TLS.html (tovuti hiyo ina msamiati wa Kimakonde)
Marejeo [hariri]
- Maho, Jouni & Bonny Sands. 2002. The languages of Tanzania: a bibliography. (Orientalia et africana gothoburgensia, no 17.) Göteborg: Acta Universitatis Gothoburgensis. Pp ix, 428. ISBN 91-7346-454-6
Kitabu hiki kinataja marejeo mengine kama:
- Liphola, Marcelino. 2001. Aspects of phonology and prosody in Shimakonde. PhD thesis. Ohio State University at Columbus.
- Lorenz, A. 1914. Entwurf einer Kimakonde-Grammatik. Mitteilungen des Seminars für orientalische Sprachen, 17 (III. Abt.), uk.46-117.
- Yukawa, Yasutoshi. 1989. A tonological study of Makonde verbs. In: Studies in Tanzanian languages (Bantu linguistics, vol 2), uk.519-560. Tokyo: Institute for the Study of Languages and Cultures of Asia and Africa (ILCAA), Tokyo University of Foreign Studies.
Viambishi ni mofimu au viungo vyenye maana ambavyo hufungamanishwa na mzizi/shina la neno ili kulipa neno hilo maana mbalimbali za kisarufi kama vile nafsi, wakati, hali, urejeshi, n.k Viambishi awali ni vile vinavyotangulia mzizi wenyewe, yaani huwa kabla ya mzizi/shina. SHINA AU MZIZI: Hakuna tofauti kati ya shina na mzizi MZIZI/SHINA, Ni sehemu ya neno inayobeba maana yake kuu na huwa haibadiliki, Kwa mfano, tuangalie vitenzi vifuatavyo: a-na-LIM-a wa-li-LIM-i-a ni-ta-LIM-iw-a wa-na-vyo-LIM-a Ukiangalia kwa makini, utaona kuna sehemu ya kitenzi hiki ambayo haibadiliki katika mifano ya hapo juu. Sehemu hiyo ni (-LIM-). Na hii ndiyo shina au mzizi wa kitenzi LIMA. Mfano mwingine: a-li-ki-SOM-a hu-SOM-ew-a wa-li-SOM-e-an-a a-li-m-SOM-e-a i-li-SOM-w-a Tunaona hapa mzizi/shina la kitenzi SOMA, ni -som- Ili utambue shina/mzizi wa kitenzi unafaa kuwazia hali mbalimbali au kauli tofautitofauti za mnyambuliko wa kitenzi halafu ubainishe sehemu isiyobadilika.