Kilumbu
Kilumbu ni lugha ya Kibantu nchini Gabon na Jamhuri ya Kongo inayozungumzwa na Walumbu. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kilumbu nchini Gabon imehesabiwa kuwa watu 19,700. Pia kuna wasemaji zaidi ya 3000 nchini Jamhuri ya Kongo. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kilumbu kiko katika kundi la B40.
Viungo vya nje [hariri]
- lugha ya Kilumbu kwenye Multitree
- ramani ya Kilumbu
- http://www.ethnologue.org/show_language.asp?code=lup
Viambishi ni mofimu au viungo vyenye maana ambavyo hufungamanishwa na mzizi/shina la neno ili kulipa neno hilo maana mbalimbali za kisarufi kama vile nafsi, wakati, hali, urejeshi, n.k Viambishi awali ni vile vinavyotangulia mzizi wenyewe, yaani huwa kabla ya mzizi/shina. SHINA AU MZIZI: Hakuna tofauti kati ya shina na mzizi MZIZI/SHINA, Ni sehemu ya neno inayobeba maana yake kuu na huwa haibadiliki, Kwa mfano, tuangalie vitenzi vifuatavyo: a-na-LIM-a wa-li-LIM-i-a ni-ta-LIM-iw-a wa-na-vyo-LIM-a Ukiangalia kwa makini, utaona kuna sehemu ya kitenzi hiki ambayo haibadiliki katika mifano ya hapo juu. Sehemu hiyo ni (-LIM-). Na hii ndiyo shina au mzizi wa kitenzi LIMA. Mfano mwingine: a-li-ki-SOM-a hu-SOM-ew-a wa-li-SOM-e-an-a a-li-m-SOM-e-a i-li-SOM-w-a Tunaona hapa mzizi/shina la kitenzi SOMA, ni -som- Ili utambue shina/mzizi wa kitenzi unafaa kuwazia hali mbalimbali au kauli tofautitofauti za mnyambuliko wa kitenzi halafu ubainishe sehemu isiyobadilika.