Kilomwe cha Malawi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Kilomwe cha Malawi ni lugha ya Kibantu nchini Malawi inayozungumzwa na Walomwe. Hakielewekani na Kilomwe cha Msumbiji. Mwaka wa 2001 idadi ya wasemaji wa Kilomwe cha Malawi imehesabiwa kuwa watu 250,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kilomwe hakiainishwi kwa vile ni mchanganyiko wa lugha ya Kinyanja ambacho kiko katika kundi la N30 na wa lugha ya Kimakua ambacho kiko katika kundi la P30.

Viungo vya nje [hariri]

Viambishi ni mofimu au viungo vyenye maana ambavyo hufungamanishwa na mzizi/shina la neno ili kulipa neno hilo maana mbalimbali za kisarufi kama vile nafsi, wakati, hali, urejeshi, n.k Viambishi awali ni vile vinavyotangulia mzizi wenyewe, yaani huwa kabla ya mzizi/shina. SHINA AU MZIZI: Hakuna tofauti kati ya shina na mzizi MZIZI/SHINA, Ni sehemu ya neno inayobeba maana yake kuu na huwa haibadiliki, Kwa mfano, tuangalie vitenzi vifuatavyo: a-na-LIM-a wa-li-LIM-i-a ni-ta-LIM-iw-a wa-na-vyo-LIM-a Ukiangalia kwa makini, utaona kuna sehemu ya kitenzi hiki ambayo haibadiliki katika mifano ya hapo juu. Sehemu hiyo ni (-LIM-). Na hii ndiyo shina au mzizi wa kitenzi LIMA. Mfano mwingine: a-li-ki-SOM-a hu-SOM-ew-a wa-li-SOM-e-an-a a-li-m-SOM-e-a i-li-SOM-w-a Tunaona hapa mzizi/shina la kitenzi SOMA, ni -som- Ili utambue shina/mzizi wa kitenzi unafaa kuwazia hali mbalimbali au kauli tofautitofauti za mnyambuliko wa kitenzi halafu ubainishe sehemu isiyobadilika.