Jakaya Kikwete
| Dk Jakaya Kikwete | |
|
|
|
| Aliingia ofisini 21 December 2005 |
|
| Waziri Mkuu | Edward Lowassa (2005-08) Mizengo Pinda |
|---|---|
| Makamu wa Rais | Ali Mohamed Shein (2005-10) Mohamed Gharib Bilal |
| mtangulizi | Benjamin Mkapa |
|
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika
|
|
| Muda wa Utawala 31 January 2008 – 2 February 2009 |
|
| mtangulizi | John Kufuor |
| aliyemfuata | Muammar al-Gaddafi |
|
|
|
| Muda wa Utawala November 1995 – 21 December 2005 |
|
| Rais | Benjamin Mkapa |
| aliyemfuata | Asha-Rose Migiro |
|
|
|
| Muda wa Utawala 1994 – 1995 |
|
| Rais | Ali Hassan Mwinyi |
| mtangulizi | Steven Kibona |
| aliyemfuata | Simon Mbilinyi |
|
Mbunge wa Tanzania
|
|
| Muda wa Utawala 1990 – 2005 |
|
| aliyemfuata | Ramadhani Maneno |
| Constituency | Bagamoyo (1990-95) Chalinze (1995-2005) |
|
|
|
| tarehe ya kuzaliwa | 7 Oktoba 1950 Msoga, Tanganyika |
| utaifa | Mtanzania |
| ndoa | Salma Kikwete |
| watoto | 8 |
| makazi | 1 Ocean Road, 11400, Dar es Salaam |
| mhitimu wa | UDSM (BA) |
| Fani yake | Mchumi |
| dini | Uislamu |
| tovuti | jakayakikwete.com |
| Military service | |
| Allegiance | Jamhuri ya Muungano wa Tanzania |
| Service/branch | Jeshi la Tanzania |
| Years of service | 1976-1992 |
| Rank | Luteni Kanali |
Jakaya Mrisho Kikwete tangu tarehe 21 Desemba 2005 ni rais wa nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Yaliyomo |
Asili [hariri]
Amezaliwa 7 Oktoba 1950 katika kijiji cha Msoga, kata ya Lugoba, tarafa ya Msoga, Jimbo la Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo, mkoa wa Pwani. Lugha ya mama ilikuwa Kikwere.
Alizaliwa katika familia ya wanasiasa. Babu yake Mzee Mrisho Kikwete alikuwa chifu wa Wakwere. Baba yake alikuwa Mkuu wa Wilaya Pangani, Same na Tanga. Jakaya Kikwete amesimulia hadithi ya kifamilia ya kuwa wakati mama yake alipokuwa mja mzito naye, Babu alitamka kuwa ikiwa mtoto atakuwa wa kiume atampatia urithi wa cheo chake.
Masomo [hariri]
1958 – 1961 akasoma Shule ya Msingi Msoga, halafu 1962 – 1965 Shule ya Middle School Lusonga, halafu Shule ya Sekondari Kibaha akiongeza A-level huko Shule ya Sekondari Tanga. Kuanzia mwaka 1972 alisoma uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akimaliza digrii yake mwaka 1978. Akajiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Jakaya aliposoma Shule ya Sekondari ya Kibaha alikuwa mwenyekiti wa wanafunzi na pia wa Vijana wa TANU. Shule ya Sekondari Tanga alikuwa Kiranja Mkuu na pia kiongozi wa timu ya mpira. UDS alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa halmashauri ya wanafunzi.
Kupanda ngazi katika siasa [hariri]
1988 akateuliwa kuwa mbunge na waziri msaidizi. 1990 alichaguliwa kuwa mbunge wa Bagamoyo/Chalinze akirudishwa kila uchaguzi hadi mw. 2000. Akawa waziri akipita katika wizara za maji na fedha.
1995 alijaribu kuchaguliwa kuwa mgombea wa uraisi upande wa CCM. Inasemekana ya kwamba Mwl. Julius Nyerere alimwomba wakati ule kumwachia Benjamin Mkapa nafasi aliyeteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM. Kikwete akawa Waziri ya Mambo ya Nje katika serikali zote mbili za Mkapa.
Mwaka 2005 alifaulu kuteuliwa mgombea wa CCM kwa nafasi ya raisi na akashinda uchaguzi wa Desemba 2005 akizoa 80% za kura zote.
Viungo vya nje [hariri]
- Jakaya Kikwete Fans Website
- Government of Tanzania
- Ippmedia Interview with Col Kikwete
- BBC Profile
- Jakaya Kikwete Swearing-In Ceremony
| Orodha ya Marais wa Tanzania | |
| Julius Nyerere • Ali Hassan Mwinyi • Benjamin Mkapa • Jakaya Kikwete |
